Ḥaqq al-Nas ((Haki za Watu) ndio mada muhimu na ambayo husisitizwa mara kwa mara katika dini ya Kiislamu kiasi kwamba aya ndefu zaidi ya Qur'ani (Surah Baqarah aya ya 282) pia imejitolea kwa mada hii, na Amirul Muuminina, Imam Ali (AS) pia anasema: "Mwenyezi Mungu, Mtukufu, anaheshimu haki za waja wake kama utangulizi wa heshima ya haki."
Aya nyingine ya Qur’ani Tukufu inasema: Walaji riba wataingia katika kundi la watu Siku ya Kiyama wakiwa kama wendawazimu, kama mlevi asiyeweza kujizuia, wataingia kwenye kundi namna hii; *Wale walao riba hawasimami ila kama anavyo simama aliye zugwa na Shet´ani kwa kumgusa. Hayo ni kwa kuwa wamesema: Biashara ni kama riba. Lakini Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na ameiharimisha riba. Basi aliye fikiwa na mawaidha kutoka kwa Mola wake Mlezi, kisha akajizuia, basi yake ni yaliyo kwisha pita, na mambo yake yako kwa Mwenyezi Mungu. Na wenye kurudia basi hao ndio watu wa Motoni, humo watadumu."
Mtukufu Mtume (SAW) amesema: "Wakati wa Miraj niliwaona watu wakati ambao hawakuweza kusimama hata wangejitahidi vipi kwa sababu ya ukubwa wa matumbo yao, nikamuuliza Jibril, ni nani hao? Akasema: “Hao ni walaji riba” na akaashiria kwenye Aya ya “Wale walao riba hawasimami….”
Ikiwa mtu ana ghera kuhusu kidini, uwezekano wa adhabu za riba unapaswa kumuuma, kwa sababu ni chungu. Ifahamike kwamba matokeo mabaya ya riba si jambo la kinadharia tu, bali ni ukweli ambao Qur'ani Tukufu inauelezakwa njia ya uhakika na ya uhakika.
Dhambi ya riba ni kubwa sana, na ukweli kwamba Qur’ani Tukufu inasema: "Walaji riba wataingia katika kundi la watu Siku ya Kiyama wakiwa kama wendawazimu", ni mfano wa matendo yao wenyewe; Kwani watu hawa duniani wanahalalisha riba kwa maneno ya kichaa na kuvaa kofia ya sharia na kusema kuna tofauti gani kati ya muamala na riba? Qur'ani Tukufu inasema vivyo hivyo katika muendelezo wa Aya tukufu: " Hayo ni kwa kuwa wamesema: Biashara ni kama riba."
Mwenyezi Mungu huharibu riba na huzidisha sadaka. Kwa maneno mengine, riba huharibu baraka, na mikopo ya hisani au Qardh al-Hasan huleta baraka kwa maisha ya mwanadamu. Uzoefu umethibitisha kwamba ikiwa mali iliyopatikana kutokana na riba haitaharibiwa wakati wa uhai wa mtoaji riba, haitawafaa warithi wake na watoto wake bali italeta ubadhirifu, itasababisha hitilafu, mgawanyiko na dhambi baina yao.
Wakati mwingine utaona watu wana mali nyingi, lakini wanaishi kwa taabu na maisha yao ni magumu kuliko masikini yeyote. Hii ni ishara ya kutokuwa na baraka na yamkini sababu ikawa ni riba.
4239570