IQNA

Benki za Kiislamu

Russia yaafiki kuidhinisha mfumo wa benki za Kiislamu

12:52 - July 16, 2022
Habari ID: 3475510
TEHRAN (IQNA) – Sheria mpya inaandaliwa nchini Russia ambayo itasimamia benki za Kiislamu nchini humo katika jitihada za kuvutia wawekezaji kutoka nchi za Kiislamu.

Gazeti la kila siku la Kirusi la Kommersant limeripoti kwamba huduma za Kiislamu za kifedha zitatolewa katika fremu ya Mashirika ya Ubia wa Kifedha (FPO) na kuwapa wateja huduma za kifedha zinazofuata sheria za Kiislamu.

Ripoti hiyo iliongeza kuwa FPOs zitakuwa chini ya Benki Kuu ya Russia, ambayo itakuwa na orodha ya mashirika yote yenye kutoa huduma hizo.

Mkuu wa Kamati ya Bunge la Russia (Duma) ya Soko la Fedha, Anatoly Aksakov, alisema kwamba rasimu ya sheria hiyo itawasilishwa hivi karibuni katika bunge kwa ajili ya kuidhinishwa.

Benki za Kiislamu zinafanya kazi chini ya miongozo ya kidini na kimaadili ambapo malipo ya riba  marufuku. Sekta ya benki za Kiislamu duniani inakua kwa asilimia 14 kila mwaka na inakadiriwa kuwa na thamani ya dola trilioni 1.99. Inachangia asilimia sita ya hisa katika sekta ya benki ya kimataifa isiyo ya Kiislamu.

Kwa mujibu wa rasimu ya sheria, mashirika hayo yanaweza kukusanya fedha kutoka kwa watu binafsi na vyombo vya kisheria na kuwekeza katika miradi kulingana na kanuni za sheria za Kiislamu kwa misingi ya ushirikiano. Benki ya Urusi, uchapishaji huo ulisema, iko tayari kwa uvumbuzi, lakini inapendelea kujaribu mfumo mpya kwenye anuwai ndogo ya vyombo kwanza.

FPOs zitakazoanzishwa Russia  zitatoa huduma zifuatazo: kutoa mikopo ya pesa kwa mashirika na watu binafsi bila kutoza ada na kufadhili biashara mmbali mbali kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu.

Wazo la kuanzisha benki ya Kiislamu nchini Urusi limejadiliwa kwa muda mrefu.

Miezi michache iliyopita Kamati ya Bunge kuhusu Soko la Fedha itaanzisha kikundi cha kazi kuhusu fedha za Kiislamu kwa lengo la kuvutia wawekezaji katika sekta ya fedha kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu na nchi nyingine za Kiislamu.

3479712

captcha