IQNA

Benki ya Kiislamu

Benki ya Kwanza ya Kiislamu ya Australia yawavutia wasio Waislamu

20:46 - October 14, 2022
Habari ID: 3475927
TEHRAN (IQNA) - Katika hatua muhimu ya kusonga mbele Waislamu 800,000 wa Australia, nchi itashuhudia benki yake ya kwanza ya Kiislamu ikifunguliwa rasmi.

Benki ya Kiislamu ya Australia imepewa leseni na Mamlaka ya Udhibiti wa Tahadhari ya Australia  hii ikiwa ni mara ya kwanza leseni kama hiyo kutolewa nchini humo.

Kuanzishwa kwa benki hiyo kunamaanisha Waislamu, ambao hawawezi kulipa au kupokea riba kutokana na mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu, sasa wanaweza kufikia lengo lao la kumiliki nyumba.

Benki ya Kiislamu ya Australia itatoa huduma mbalimbali kwa wateja Waislamu, ikiwa ni pamoja na fedha za kununua nyumba, akiba na akaunti za kila siku.

Itafanya jaribio na idadi ndogo ya wateja, kabla ya kufungua milango kwa wote, na tayari watu 8,000 wako kwenye orodha ya wanaosubiri.

Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Dean Gillespie, alisema mtindo wake wa ufadhili wa kununua nyumba utakuwa ‘umiliki wa pamoja’, akimaanisha wateja watatozwa kodi wakati wanaishi katika nyumba  badala ya kulipa riba.

“[Mteja] anaweza kuanza na amana ya asilimia 20…hiyo ina maana kwamba wataanza kumiliki asilimia 20 ya nyumba, na benki itamiliki asilimia 80 nyingine,” alisema.

"Tunachoruhusu [mteja] kufanya ni kununua hisa zaidi za mali hiyo kwa wakati."

Hisa ya mpangaji katika mali huongezeka wanapolipa kodi, hadi awe mmiliki kamili wa nyumba.

Chini ya imani ya Kiislamu, benki hiyo pia imepigwa marufuku kushughulika na sekta zikiwemo za pombe na kamari.

Gillespie alisema pia watafanya biashara na mashirika ya kbiashara ambayo yanazingatia sera za kutunza mazingira

"Tunasikia hadithi kuhusu watu kuweka pesa chini ya kitanda au kwenye masanduki maalumu nyumbani kwa sababu hawajafurahi kuziweka kwenye mfumo wa kawaida wa benki," alisema.

"Hilo ni jambo ambalo tunatarajia sana kurekebisha."

Benki hiyo imeweza kuwavutia wasio Waislamu pia, huku watu wakipendelea mfumo wa kununua nyumba kwa njia kukodisha badala ya riba.

"Tunapata maswali mara kwa mara kutoka kwa Waustralia ambao wameishi Mashariki ya Kati ... na wamewahu kutumia mfumo wa Kiislamu wa fedha," alisema.

Amebaini kuwa wateja hao wasio Waislamu wako katika orodha ya kungojea na wanasema wanavutia na msingi wa maadili katika benki za Kislamu.

Leseni ya Benki ya Kiislamu ya Australia ina masharti kwani inairuhusu kujaribu bidhaa na idadi ndogo ya wateja kwa kipindi cha  miaka miwili, kabla ya kutuma maombi ya leseni kamili.

3480841

captcha