Matukio machungu yalitokea katika miezi ya mwisho ya maisha yenye baraka ya Hadhrat Zahra (SA na machungu na matatizo aliyopitia baada ya kufariki kwa Mtukufu Mtume (SAW) yalikuwa kiasi kwamba kwa mujibu wa vyanzo vya kihistoria, hakuna mtu aliyemuona akicheka katika kipindi hicho.
Khutba ya Fadakiyah iliyobaki tangu wakati huo ni uthibitisho wa matatizo na machungu hayo. Hotuba iliyotolewa na Hadhrat Zahra (SA) mbele ya Maswahaba (maswahaba wa Mtukufu Mtume SAW) inafichua wazi yale aliyopitia baada ya Mtume (SAW). Kumpoteza baba yake, tukio la Saqifah, matukio yanayohusiana na ukhalifa na kutekwa kwa Fadak vilikuwa sehemu ya sababu zilizopelekea huzuni hii.
Upinzani wa Hadhrat Zahra (SA) na Imam Ali (AS) kwa uamuzi wa Saqifah ulipelekea kutishiwa kwao. Baada ya wao kukataa kutoa kiapo cha utii kwa Khalifa wa wakati huo, nyumba yao ilishambuliwa, ambapo Hazrat Zahra (SA) alijeruhiwa na mimba yake iliharibika. Aliugua na akafa kishahidi muda mfupi baadaye.
Hadhrat Zahra (SA) alimuomba a Imam Ali (AS) kwamba ahakikishe wale wanaompinga wasihudhurie mazishi yake. Alimwomba amzike usiku. Kwa mujibu wa ripoti maarufu, Hadhrat Zahra (SA) aliuawa kishahidi huko Madina mnamo tarehe 3 ya mwezi wa mwandamo wa Jumada al-Thani mwaka wa 11 baada ya Hijra. Umri wake wakati wa kifo cha kishahidi unasemekana kuwa ulikuwa miaka 18, wakati kwa mujibu wa Hadith kutoka kwa Imam Baqir (SAW), alikuwa na miaka 23 alipouawa kishahidi.
3490970