Miongoni mwao walikuwemo Omar, Abu Bakr, Abdul Rahman ibn Ouf, na wengineo. Hadhrat Ali (AS) pia alikuwa tayari sana kumuoa Hadhrat Zahra (SA) kwa sababu ya uhusiano wao wa karibu wa kifamilia na fadhila za binti huyo wa Mtume (SAW), lakini kwa mujibu wa wanahistoria, hakutubutu mwenyewe binafsi kuenda kumposa.
Lakini Saad ibn Ma’az alizungumza na Mtume (SAW) kuhusu hilo na Mtume (SAW) akakubali ndoa ya Ali (AS) na Hadhrat Zahra (SAW).
Kama Muhajirina wengine, Ali (AS) alikuwa na hali ngumu ya kiuchumi katika miezi ya kwanza baada ya kuhama. Kwa hiyo, kwa mapendekezo ya Mtukufu Mtume (SAW) aliuza silaha zake na akafanya pesa hizo kuwa mahari ya Hadhrat Zahra (SAW).
Hafla ya ndoa yao ilifanyika katika Msikiti wa Mtume kwa kushirikisha Waislamu.
Kipindi cha kwanza cha ndoa yao kiliambatana na hali ngumu ya kiuchumi, kiasi kwamba wakati mwingine walikosa hata chakula cha kuwalisha watoto wao. Hata hivyo, Hadhrat Zahra (SA) hakulalamika kwa mumewe na wakati mwingine alisuka pamba ili kumsaidia mumewe kupata riziki.
Kwa kuzingatia pendekezo la Mtume, Hadhrat Zahra (SA) alikuwa tayari kufanya kazi za nyumbani na kumwacha Ali (AS) afanye kile kilichohitajika kufanywa nje ya nyumba. Mtukufu Mtume (SAW) alipomtuma Fidda kama mtumishi, Hadhrat Zahra (SA) alifanya nusu ya kazi za nyumbani na Fidda alifanya iliyobaki.
Ali (AS) alimheshimu sana Hadhrat Zahra (SA). Kwa mujibu wa Hadith, Hadhrat Ali (AS) alisema kwamba Zahra (SA) hakuwahi kumkasirisha wala hakumkasirisha Zahra (SA).
Vyanzo vya Shia na Sunni vinakubaliana kwamba wanandoa hao walikuwa na watoto wanne: Hassan, Hussein, Zeynab na Umm Kulthum. Kwa mujibu wa riwaya za madhehebu ya Shia na baadhi ya vyanzo vya Sunni, walikuwa na mtoto mwingine wa kiume, aitwaye Muhsin au Muhassin.
Inaarifiwa kuwa mimba ya Muhsin iliharibika kutokana na majeraha ambayo Bibi Zahra (SA) alipata wakati wa matukio ya baada ya kufariki kwa Mtukufu Mtume (SAW).
Hadhrat Zahra (SA) alikuwa na shughuli nyingi za kijamii na alichukua nyadhifa nyingi za kisiasa. Kuhamia Madina, akiponya majeraha ya baba yake wakati wa Vita vya Uhud, ambapo akiwa pamoja na Safiya waliwalaani waliomuua shahidi Hadhrat Hamza. Alimpelekea chakula Mtume (SAW) wakati wa Vita vya Khandaq na kuandamana naye wakati wa kutekwa kwa Makka. Hizi ni baadhi ya shughuli zake kabla ya kufariki Mtume Muhammad (SAW).
3490962