Alizaliwa mwaka 1913 katika familia maskini ya Kiislamu katika mji wa Jinan katika mkoa wa Shandong mashariki mwa China.
Ismail alisoma Uislamu katika Shule ya Kiislamu ya Changda na alipelekwa na shule hiyo katika Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al-Azhar nchini Misri baada ya kuhitimu mwaka wa 1932.
Wakati wa masomo yake huko Misri, alikuwa akihudhuria mara kwa mara vikao vya usomaji wa Qur'ani katika Msikiti wa Al-Azhar.
Vile vile alisoma Qur'ani Tukufu na alirekodi qiraa yake kwenye kanda.
Alirudi China baada ya kuhitimu kutoka Al-Azhar mnamo 1932.
Huko China alianza kufundisha lugha ya Kiarabu katika Shule ya Kiislamu ya Changda na baadaye katika taasisi ya Kiislamu huko Beijing.
Pia aliwahi kuwa mhariri mkuu wa Jarida la Nadhara al-Hilal ambalo lilichapishwa na Shule ya Kiislamu ya Changda.
Ismail alitoa wito wa marekebisho ya ufundishaji wa Kiarabu nchini China na kujumuisha kusoma magazeti ya Kiarabu kwa wale wanaosoma lugha ya Kiarabu.
Mnamo 1950, aliteuliwa kama Imamu wa Msikiti wa Fuyulu huko Shanghai na alihudumu katika jukumu hilo kwa miaka mitatu.
Pamoja na kuongoza sala za jamaa, alikuwa akifundisha masomo ya kidini na kusoma Qur'ani msikitini.
Kuanzia 1953 hadi alipostaafu mnamo 1987, alifundisha Kiarabu katika kitivo cha lugha za mashariki katika Chuo Kikuu cha Beijing.
Huko, alifunza kizazi cha wanafunzi mashuhuri katika uwanja wa lugha na utamaduni wa Kiarabu.
Aliandika idadi ya vitabu, vikiwemo kamusi ya Kiarabu hadi Kichina, kitabu kuhusu Seerah ya Mtukufu Mtume (SAW) na tafsiri ya akaunti ya safari ya Ibn Battuta.
Katika miaka yake ya 80, Ismail alianza kuhakiki tafsiri au tarjuma za Qur'an katika Kichina na vitabu maarufu vya Tafsir (Tafsiri ya Qur'ani) katika Kiarabu. Kisha akaanza kutafsiri Qur'ani Tukufu kwa Kichina.
Alikamilisha kazi hiyo lakini alifariki akiwa na umri wa miaka 88 mwaka wa 2005 kabla ya kuchapishwa.
Tafsiri yake ilichapishwa na Nations Publishing House huko Ningxia baadaye mwaka huo na kuchapishwa tena mwaka wa 2016.
3491038