IQNA

Turathi ya Kiislamu

Nakala ya kale zaidi ya Qur’ani Tukufu nchini China iko katika Msikiti wa Jiezi

21:44 - August 20, 2022
Habari ID: 3475650
TEHRAN (IQNA) - Kuna msikiti kaskazini-magharibi mwa Uchina ambao una nakala ya kale zaidi ya Qur'ani katika nchi hiyo ya Asia Mashariki.

Msahafu huo uko katika Msikiti wa Jiezi, msikiti wa pili kwa ukubwa huko Qinghai, ulioko katika kijiji cha sanlanbahai, Kitongoji cha Jiezi, Kaunti yenye mamlaka ya ndani ya Xunhua Salar.

Msahafu huo una kurasa 867 na unajumuisha Juzuu(sehemu) zote 30 za Qur’ani Tukufu.

Wataalamu wanaamini kwamba msahafu huo ni wa karne ya 8 hadi 13 Miladia. Wanasema makabila ya Kituruki yanayojulikana kama watu wa Salar walileta msahafu huo kutoka Asia ya Kati miaka 800 iliyopita.

Mwaka 2007, serikali ya China ilitenga bajeti kwa ajili ya kuutunza Msahafu huo na ilibidi  baada ya miaka mingi ya kuchakaa.

Mnamo 2009, serikali ya China iliujumuisha Msahafu huo katika orodha ya vitu vya thamani vya turathi ya kitaifa.

Katika mwaka huo huo, jumba la makumbusho lilianzishwa kwenye Msikiti wa Jiezi ambapo Msahafu huo umewekwa kwenye sanduku maalum la glasi ili kuulinda kwa kudumisha hali inayotakikana ya joto na unyevu.

Katika jumba hilo la makumbusho pia kuna nakala kadhaa zilizochapishwa za Qur’ani Tukufu zinazoonyesha sifa za maandishi ya Kichina.

Oldest Quran Manuscript in China at Jiezi Mosque

Oldest Quran Manuscript in China at Jiezi Mosque

Oldest Quran Manuscript in China at Jiezi Mosque

3480167

Kishikizo: china msahafu kale
captcha