IQNA

Kaburi la Bibi Zainab (A.S) limefungwa kwa sababu ya mashambulizi ya mara kwa mara

14:39 - February 03, 2025
Habari ID: 3480153
IQNA – Kaburi Tukufu la bibi  Zainabu (A.S.) lililoko pembezoni mwa Damascus limefungwa kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara yaliyofanywa na watu wasiojulikana.

Pia, kuswali katika eneo hili la ziara kumesitishwa ili kuzuia Fitna (machafuko) yanayosababishwa na baadhi ya watu. 

Uamuzi huu umetangazwa na maafisa wa ngazi za juu, kulingana na ripoti ya Baghdad al-Yawm.

Inaripotiwa kuwa hivi karibuni, watu wasiojulikana walijaribu kuzua machafuko na hali ya kutokuwa na usalama katika maeneo ya makaburi matakatifu.

Kwa kuongezeka kwa uwepo wa vikundi vya Hay’at Tahrir al-Sham (HTS) nchini Syria, wasimamizi wa kaburi la Bibi Zainabu (A.S.) wamekabiliwa na changamoto nyingi.

Mnamo Januari 11, idara ya ujasusi ya serikali mpya ya Syria ilitangaza kuwa imefanikiwa kuzuia shambulizi la Daesh (ISIL/ISIS) la kulipua bomu katika makamuu hayo.

Awali, HTS iliondoa wanajeshi zaidi ya 90 kutoka vikosi vyake vya kimataifa vilivyokuwa vinashika doria karibu na makamuu hayo katika vitongoji vya Damascus, kutokana na tabia mbaya na ongezeko la malalamiko dhidi yao.

Licha ya msimamo mkali wa HTS na historia yake katika masuala haya, baada ya kuchukua mamlaka nchini Syria, inasemekana kuwa inashughulikia maeneo ya kidini, hususan maeneo matakatifu ya Kishia, kwa tahadhari kubwa ili kuepuka uchokozi au uvunjaji heshima unaoweza kuzua hasira za umma.

 

 

https://iqna.ir/en/news/3491713

 

 

captcha