Wakati wa mwezi huu, watu wengi na mashirika ya hisani nchini Oman hufanya kazi kwa bidii kukusanya michango na kusaidia wale wanaohitaji. Aidha, Ramadhani ni moja ya miezi yenye shughuli nyingi za mauzo nchini.
Ramadhani nchini Oman ni mwezi ambao unajulikana kwa ununuzi wa bidhaa maalumu za mwezi huu, futari za pamoja katika misikiti, kuswali swala za Taraweeh, kusoma Qur'ani, na kuandaa matukio yanayoitwa masoko ya Qarnqashoo na Habatat.
Wakati Ramadhani inakaribia, raia wa Omani wanangoja kwa hamu tangazo la kuanza kwa mwezi huu mtukufu. Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini ndiyo inayohusika na kutazama mwezi.
Mara tu mwezi wa Ramadhani unapoandama, watu hukusanyika katika misikiti kwa ajili ya swala za Isha na Taraweeh, na baada ya swala hizi, wanakutana na kupongezana. Aidha, siku mbili hadi tatu kabla ya kuanza kwa Ramadhani, wanatembeleana na kudumisha uhusiano wa kifamilia.
Moja ya desturi muhimu za raia wa Omani wakati wa Ramadhani ni kuandaa iftar au futari za pamoja katika misikiti na kukusanya wanafamilia katika nyumba ya jamaa mkubwa, ambapo vijana na wazee hukutana pamoja kwenye meza ya futari.
Wengi hufuturu kwa maji na tende, au mtindi, pamoja na vyakula vingine vilivyotengenezwa nyumbani. Maji na tende ni muhimu kwa Waoamani, desturi ambayo ina mizizi katika uhusiano wao na mti wa tende.
Vyakula vingine ambavyo Waomani huweka kwenye meza zao wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ni Khabeesa aina ya chakula kitamu Kiomani.
Wanaofunga hushiriki katika vikao vya kusoma Qur'ani na mihadhara katika misikiti wakati wa mwezi mtukufu, hasa baada ya sala za asubuhi na alasiri.
Katikati ya Ramadhani, baadhi ya miji nchini Oman huwa na desturi ambapo watoto husherehekea tukio linaloitwa Qarnqashou katika mitaa yao. Tukio hili linasherehekewa kwa majina tofauti katika nchi kadhaa za Kiarabu katika eneo la Ghuba ya Uajemi; kwa mfano, linajulikana kama Qarqiaan nchini Saudi Arabia.
Wakati wa mwezi huu, familia za Omani zinawapa watoto wao walimu wa Kiarabu ili wajifunze Qur'ani, na kabla ya kumalizika kwa Ramadhani, sherehe inayoitwa Tumineh hufanywa ili kuwapongeza wahifadhi wa Qur'ani. Nyimbo maalum huimbwa wakati wa tukio hili.
Katika siku za mwisho za Ramadhani, masoko yanayoitwa Habbat huandaliwa na wakazi wa kila mtaa na jiji wanajua wakati masoko haya yanapofanyika. Masoko haya yanatoa vitu vinavyohitajika kwa ajili ya kusherehekea Eid al-Fitr, na kila mwaka yanavutia umati mkubwa kutoka kwa raia wa Omani.
3492462/