IQNA

Washiriki 170 katika hatua ya kwanza ya Mashindano ya Qur’an Tukufu Oman

18:49 - December 27, 2025
Habari ID: 3481720
IQNA – Takriban washiriki 170 wameingia katika hatua ya mwanzo ya mashindano ya kitaifa ya kuhifadhi Qur’an Tukufu nchini Oman.

Wizara ya Awqaf na Mambo ya Kidini ya nchi hiyo siku ya Alhamisi iliandaa hafla ya kuhitimisha duru za awali za mashindano ya kuhifadhi Qur’ani Tukufu yanayojulikana kwa jina la “Fastamsik” (Shikamana Imara).

Mashindano haya yanalenga kukuza heshima na uangalizi unaotolewa kwa Qur’ani Tukufu, kuunga mkono madrasa za Qur’ani kama nguzo za elimu na imani, kuonyesha juhudi za taasisi za wakfu na kusisitiza mchango wao katika kuendeleza ujumbe wa Qur’ani Tukufu.

Aidha, mashindano haya yanakusudia kuwaandaa washiriki kushiriki vyema katika mashindano ya Qur’ani ya ndani na ya kimataifa, na kuimarisha roho ya imani miongoni mwao kwa namna inayoinua thamani za ikhlasi na bidii.

Lengo jingine ni kuwahimiza vijana wa Oman kuwa karibu zaidi na Qur’ani Tukufu—kupitia kuhifadhi, kuelewa na kutafakari—ili wawe mifano bora ya maadili na kazi.

Mashindano haya yanajumuisha vituo vitano vya usimamizi katika mikoa ya Sultanate ya Oman, ikiwemo: Mkoa wa Dhofar, Mkoa wa Al Buraimi, Mkoa wa A’Sharqiyah Kaskazini, Mkoa wa A’Dakhiliyah na Mkoa wa Muscat.

3495855

Habari zinazohusiana
Kishikizo: qurani tukufu oman
captcha