IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Waziri wa Oman awaenzi washindi wa Mashindano ya Qur’ani ya Sultan Qaboos

20:46 - December 27, 2022
Habari ID: 3476315
TEHRAN (IQNA) - Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kidini wa Oman amewaenzi washindi wa Duru ya 30 ya Mashindano la Sultan Qaboos la Kuhifadhi Qur'ani Tukufu.

Mohammed Said Al Maamari aliongoza hafla hiyo iliyofanyika katika Msikiti Mkuu wa Sultan Qaboos.

Mashindano hayo yanalenga kuwahimiza vijana wa Oman kuhifadhi Qur'ani Tukufu na kuzingatia mafundisho yake.

Pia yanalenga kutayarisha kizazi cha wasomaji wa Qur'ani Tukufu ambao wanaweza kutumika kama kipengele cha marekebisho ya kijamii na kufundisha Qur'ani Tukufu kwa mujibu wa kanuni zilizowekwa na wanachuoni na wasomaji imara.

Mgeni rasmi alikabidhi zawadi kwa washindi wa ngazi 7 wa Mashindano ya Sultan Qaboos ya Kuhifadhi Qur'ani Tukufu 2022. Aidha aliwatunuku zawadi pia majaji katika mashindano hayo na washiriki wa kategoria ya  walemavu.

Daraja za mashindano hayo zilikuwa kama ifuatavyo: Kuhifadhi Qur'ani Tukufu nzima, kuhifadhi juzuu 24 mfululizo, kuhifadhi juzuu 18 mfululizo, kuhifadhi juzuu 12 mfululizo, kuhifadhi juzuu  6 mfululizo, kuhifadhi juzuu  4 mfululizo na kuhifadhi juzuu  2 mfululizo. Jumla ya washindani  2,881 walishiriki katika mashindano hayo mwaka huu.  Mashindano hayo ya  Qur'ani huandaliwa kila mwaka na Kituo Kikuu cha Utamaduni na Sayansi cha Sultan Qaboos Katika  Kasri ya Kifalme.

3481843

captcha