IQNA

Diplomasia

Rais Pezeshkian: Iran imechukua hatua kueneza amani baina ya nchi zote za Kiislamu

23:25 - December 30, 2024
Habari ID: 3479977
IQNA-Rais Masoud Pezeshkian ameeleza kuwa mtazamo na hatua za kivitendo za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni za kueneza amani na kudumisha usalama katika ukanda huu na baina ya nchi zote za Kiislamu; na ametaka kuwepo ushirikiano mkubwa zaidi kati ya Iran na Oman katika uwanja huo.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo Jumatatu amekutana na kufanya mazungumzo na Sayyid Badr Albusaidi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman aliyeambatana na ujumbe wa ngazi ya juu wa nchi yake kufanya ziara hapa Iran. Katika mazungumzo hayo, Rais Pezeshkian ameutaja uhusiano wa nchi hizi mbili kuwa ni mkongwe, mwema na wa kirafiki na kwamba uhusiano huo umeimarika pakubwa katika nyanja mbalimbali."   

Rais Masoud Pezeshkian amesema, kuendelea kuimarika uhusiano huo ni muhimu sana kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. 

Rais Pezeshkian ameashiria pia makubaliano yaliyofikiwa na nchi mbili za Iran na Oman kwa ajili ya kuitisha kikao kijacho cha Kamisheni ya Pamoja ya Ushirikiano wa Kiuchumi siku chache zijazo na kuongeza kuwa: Hatua nzuri za kufuatilia kikao hicho zinaendelea ili kuandaa utangulizi wa kutekelezwa mapatano yaliyofikiwa huko nyuma na pia kufanikisha mapatano mengine mapya kati ya nchi mbili. 

Katika mazungumzo hayo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman pia amewasilisha salamu za Sultan wa nchi hiyo kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, kwa Rais na wananchi wa Iran na kusema: Nchi mbili za Iran na Oman zina uhusiano wa siku nyingi na wa kihistoria ambao umejengeka juu ya misingi ya maelewano na nia njema na hivyo kuzidi kuwa imara. Amesema Sultan wa Oman anapenda sana kuimarishwa uhusiano kati ya nchi mbili hizi. 

3491271

Habari zinazohusiana
captcha