IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya Qur'ani ya Sultan Qaboos wa Oman yaanza

13:25 - August 21, 2022
Habari ID: 3475656
TEHRAN (IQNA) – Hatua ya awali ya Mashindano ya Qur'ani Tukufu ya Sultan Qaboos imeanza nchini Oman siku ya Jumatatu.

Zaidi ya wagombea 2,880 kutoka katika nchi hiyo ya Kiarabu ya Ghuba ya Uajemi watashiriki katika shindano hilo.

Wanaoandaa mashindano wanasema washiriki ni kutoka katika vituo 25 katika majimbo tofauti ya Oman.

Mashindano hayo ya Qur'ani ni ya 30 tokea yaanze kufanyika kila mwaka na huandaliwa na Kituo cha Juu cha Utamaduni na Sayansi cha Sultan Qaboos katika Kasri ya Kifalme.

Miongoni mwa malengo muhimu zaidi ya mashindano hayo ni kuwahimiza Waomani kuhifadhi na na kufuata mafundisho ya Qur'ani, kuinua kizazi cha Qur'ani, kubaini vipaji vyawasomaji Qur'ani Tukufu  na kuimarisha hadhi ya Oman katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani.

Kategoria za  mashindano hayo ya Qur'ani ni kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu, kuhifadhi Juzuu 18, kuhifadhi Juzuu12, kuhifadhi Juzuu sita (kwa wale waliozaliwa 2007 na baadaye), kuhifadhi Juzi nne, na Juzi mbili ni kategoria.

Oman ni nchi iliyoko Kusini Magharibi mwa Asia, ikipakana na Bahari ya Arabia, Ghuba ya Oman, na Ghuba ya Uajemi, na iko kati ya Yemen na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE). Takriban Waomani wote ni Waislamu.

3480172

captcha