IQNA

Wanazuoni wa Kiislamu duniani watoa Fatwa kuharamisha mahusiano na Israel

13:37 - January 21, 2026
Habari ID: 3481830
IQNA – Umoja wa Kimataifa wa Wanazuoni wa Kiislamu (International Union of Muslim Scholars – IUMS) umetoa fatwa (hukumu ya kidini) ikitangaza kwamba kuwa na mahusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel ni haramu kisheria kwa mujibu wa Uislamu.

Tangazo hilo lilitolewa wakati wa kikao cha sita cha Baraza la Wadhamini wa IUMS kilichofanyika mjini Istanbul tarehe 18–19 Januari, kwa mujibu wa ripoti ya Arabi 21.

Baraza la Wadhamini la IUMS lilijadili masuala kadhaa nyeti yanayohusu ulimwengu wa Kiislamu pamoja na maendeleo ya sasa ya kimataifa.

Kikao hicho kiliongozwa na Katibu Mkuu wa IUMS, Dkt. Sheikh Ali Al-Qaradaghi.

Katika hotuba yake, Sheikh Al-Qaradaghi alisisitiza nafasi ya umoja huo, wanazuoni na wahubiri katika kuinua jamii za Kiislamu na kulinda maadili ya kidini na ya kibinadamu, hasa katika mazingira ya changamoto kama mashambulizi dhidi ya maeneo matakatifu, kudhibiti maumbile ya asili ya binadamu, pamoja na kuenea kwa misimamo mikali, ukana Mungu, na ukiukwaji wa mikataba ya kimataifa.

Kuhusu utawala wa Kizayuni, IUMS ilizitaka nchi za Kiislamu na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) kuchukua msimamo wa pamoja na wa umoja katika kuunga mkono Palestina katika majukwaa ya kimataifa.

Umoja huo pia ulisifu juhudi za kikanda na kimataifa za kulinda umoja na utulivu wa Yemen, kuunga mkono uhalali wa serikali ya Sudan, na kuwalinda Waislamu wachache wanaodhulumiwa katika maeneo mbalimbali duniani.

Habari inayohusiana:

IUMS ililaani vitendo vya uchokozi na uingiliaji wa kijeshi katika masuala ya ndani ya mataifa huru.

Ikilaani vikali uchochezi wa chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) unaolenga taasisi za Kiislamu zenye msimamo wa kati katika nchi za Magharibi, umoja huo ulisisitiza umuhimu wa kuwepo kwa ufafanuzi wa kisheria unaokubalika kimataifa kuhusu ugaidi wa dola na wa watu binafsi, pamoja na kuzingatia mitaala sahihi ya elimu ya Kiislamu ili kulinda utambulisho, utamaduni na maadili ya Kiislamu.

4329507

captcha