Katibu Mkuu wa IUMS, Sheikh Ali al-Qaradaghi, ametoa tamko rasmi la kuunga mkono wananchi wa Ukanda wa Gaza, akisisitiza kuwa kulinda damu ya watoto, wanawake na wanaume wa Gaza mbele ya vita vya mauaji ya halaiki vinavyoendeshwa na utawala wa Kizayuni ni jukumu la Ummah wa Kiislamu.
Ifuatayo ni sehemu ya tamko la Sheikh al-Qaradaghi:
…Ndiyo, damu ya watoto, wanawake na wazee wa Gaza pia imo mabegani mwa Ummah wetu.
Jihadi ya aina yoyote ya kuwaokoa ni faradhi juu ya serikali zetu.
Komesheni njaa Gaza... Komesheni mauaji ya halaiki sasa.
Natoa wito kwa serikali za Ummah wa Kiislamu na kwa kila mtu mwenye uwezo miongoni mwa mataifa ya Kiislamu, kuanzisha jihadi ya kila aina kwa mali, nafsi, maneno na vitendo ili kuokoa maisha ya watu wasio na hatia walioko ndani ya mzingiro unaowakandamiza na mauaji ya kimfumo yanayoendelea Gaza.
Kile kinachotokea Gaza leo siyo tu vita, bali ni jinai ya kiwango kikubwa: mzingiro kamili, njama ya kuwanyima chakula, na mauaji ya raia kwa makusudi. Gaza imegeuka kuwa gereza lisilo na chakula, dawa wala maji.
Yeyote mwenye uwezo wa kuwasaidia waliodhulumiwa hawa lakini akakaa kimya, amevunja ahadi ya udugu na dini, na anastahili onyo kali la Mwenyezi Mungu aliyesema:
“Na Malaika watawaambia wale waliozidhulumu nafsi zao: ‘Mlikuwa katika hali gani?’ Watasema: ‘Tulikuwa wanyonge katika ardhi.’ Malaika watasema: ‘Je, ardhi ya Mwenyezi Mungu haikuwa pana mpaka muhamie ndani yake?’ Hao makaazi yao ni Jahannamu, na huo ni mwisho muovu.”(Surat An-Nisa, aya ya 97)
Na Mwenyezi Mungu pia amesema:
“Wakomesheni. Bila shaka watasailiwa.”(Surat As-Saaffat, aya ya 24)
Huu ni wakati wa maamuzi, kati ya aibu na ushindi, kati ya kushindwa na wajibu. Taifa lisilosimama kwa ajili ya Gaza leo litapoteza heshima kabla halijapoteza nafasi yake katika historia.
Enyi Ummah wa Kiislamu, saidieni Gaza sasa kwa kila mllichonacho, kwani umwagaji damu hausubiri, njaa haingoji, na maisha ya watu hayawezi kurudi.
Wanazuoni wa Kiislamu duniani wataka mataifa ya Kiislamu kuisaidia Gaza
IQNA – Umoja wa Kimataifa wa Wanazuoni wa Kiislamu (IUMS) umetoa wito kwa serikali za Kiislamu na mataifa ya Waislamu kuchukua hatua na kufanya jihadi ili kuisaidia Gaza na kuwaokoa watu wasio na hatia walioko chini ya mzingiro wa Israel katika Ukanda wa Palestina.
Katibu Mkuu wa IUMS, Sheikh Ali al-Qaradaghi, ametoa tamko rasmi la kuunga mkono wananchi wa Ukanda wa Gaza, akisisitiza kuwa kulinda damu ya watoto, wanawake na wanaume wa Gaza mbele ya vita vya mauaji ya halaiki vinavyoendeshwa na utawala wa Kizayuni ni jukumu la Ummah wa Kiislamu.
Ifuatayo ni sehemu ya tamko la Sheikh al-Qaradaghi:
…Ndiyo, damu ya watoto, wanawake na wazee wa Gaza pia imo mabegani mwa Ummah wetu.
Jihadi ya aina yoyote ya kuwaokoa ni faradhi juu ya serikali zetu.
Komesheni njaa Gaza... Komesheni mauaji ya halaiki sasa.
Natoa wito kwa serikali za Ummah wa Kiislamu na kwa kila mtu mwenye uwezo miongoni mwa mataifa ya Kiislamu, kuanzisha jihadi ya kila aina kwa mali, nafsi, maneno na vitendo ili kuokoa maisha ya watu wasio na hatia walioko ndani ya mzingiro unaowakandamiza na mauaji ya kimfumo yanayoendelea Gaza.
Kile kinachotokea Gaza leo siyo tu vita, bali ni jinai ya kiwango kikubwa: mzingiro kamili, njama ya kuwanyima chakula, na mauaji ya raia kwa makusudi. Gaza imegeuka kuwa gereza lisilo na chakula, dawa wala maji.
Yeyote mwenye uwezo wa kuwasaidia waliodhulumiwa hawa lakini akakaa kimya, amevunja ahadi ya udugu na dini, na anastahili onyo kali la Mwenyezi Mungu aliyesema:
“Na Malaika watawaambia wale waliozidhulumu nafsi zao: ‘Mlikuwa katika hali gani?’ Watasema: ‘Tulikuwa wanyonge katika ardhi.’ Malaika watasema: ‘Je, ardhi ya Mwenyezi Mungu haikuwa pana mpaka muhamie ndani yake?’ Hao makaazi yao ni Jahannamu, na huo ni mwisho muovu.” (Surat An-Nisa, aya ya 97)
Na Mwenyezi Mungu pia amesema:
“Wakomesheni. Bila shaka watasailiwa.” (Surat As-Saaffat, aya ya 24)

3493932