IQNA

Kadhia ya Palestina

Fatwa ya IUMS: Mataifa ya Kiislamu yanapaswa kuchukua hatua kuokoa Gaza

18:15 - November 01, 2023
Habari ID: 3477825
DOHA (IQNA) - Muungano wa Kimataifa wa Wanazuoni wa Kiislamu (IUMS) ulitoa fatwa siku ya Jumanne, ukizitaka nchi za Kiislamu kuingilia kati ili kuwaokoa watu wa Gaza kutokana na mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na utawala haramu wa Israel.

Kamati ya Fatwa ya IUMS ilitoa taarifa ya "kutangaza ukweli na kueleza wajibu wa Umma kwa kile kinachotokea kwa watu wetu huko Gaza ambapo mashambulizi ya anga ya Israeli yamepelekea watu zaidi ya 8000 kuuawa, hasa wanawake na watoto , katika siku 25 zilizopita.

"Serikali na majeshi rasmi (ya nchi za Kiislamu) yana wajibu wa kisheria kuingilia kati kwa haraka na kuokoa Gaza kutokana na mauaji ya kimbari na uharibifu," inasomeka Fatwa hiyo ambayo imeongeza kwamba, "Lazima waiunge mkono Palestina kulingana na wajibu wao wa kidini, kisiasa, kisheria na kimaadili, pamoja na kimataifa, na pia kwa mujibu wa  maslahi ya kimkakati ya kanda na ya umma.”

Pia ilisisitiza kwamba "uingiliaji kati wa kijeshi na usambazaji wa zana za kijeshi na utaalamu unaohitajika kisheria kwa Wapalestina wote ndani ya maeneo yanayokaliwa na waliot katika nchi nne jirani, kuanzia Misri, Jordan, Syria na Lebanon.

Zaidi ya hayo, mkutano na waandishi wa habari ulifanyika katika makao makuu ya Umoja wa Kimataifa wa Wanazuoni wa Kiislamu mjini Doha, Qatar, baadaye mchana, na kuhudhuriwa na wanazuoni wengi wa umoja huo, wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Umoja huo, Katibu Mkuu wa IUMS Sheikh Dr Ali Mohiuddin Ali Al Qaradaghi

Mkutano huo ulisisitiza haja kubwa ya uingiliaji kati wa haraka na kutumwa misaada ya dharura ya kibinadamu ili kuinusuru Gaza kutokana na mauaji ya kimbari na uharibifu kamili unaoikabili.

Wito wa kuisaidia Palestina ulithibitishwa tena kama jukumu la kisheria na jukumu la Kiislamu na la kibinadamu, na katazo la wazi dhidi ya kukaa kimya mbele ya uchokozi bila kujibu.

3485834

Habari zinazohusiana
captcha