Ali Muhammad al-Salabi pia alizitaka nchi nyingine za dunia kuchukua hatua kukomesha vita katika nchi hiyo ya Kiafrika na kukabiliana na athari zake mbaya..
Alisema, Waislamu zaidi ya wengine wanatakiwa kuwa na jukumu la kukomesha vita hivi na kuwasaidia watu wa Sudan, huku akiashiria Aya ya 9 ya Surah Al-Hujurat ya Quran: “Na ikiwa makundi mawili katika Waumini yanapigana, basi yapatanisheni. Na likiwa moja la hao linamdhulumu mwenzie, basi lipigeni linalo dhulumu mpaka lirejee kwenye amri ya Mwenyezi Mungu. Na likirudi basi yapatanisheni kwa uadilifu. Na hukumuni kwa haki. Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wanao hukumu kwa haki.”
Akizungumzia matamshi ya mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Tedros Adhanom Ghebreyesus kuhusu hali nchini Sudan, alisema mfumo wa afya nchini humo umeporomoka.
Al-Salabi alibainisha kuwa uingiliaji wa kigeni unafanyika katika mzozo wa Sudan, akionya kwamba ajinabi hawa hawatakii mema Sudan, Afrika, na ulimwengu wa Kiislamu.
Akiwa ziarani nchini Sudan siku ya Jumapili, Ghebreyesus alionya kwamba ukubwa wa hali ya hatari ni wa kushtua.
Aliuambia ulimwengu "kuamka na kuisaidia Sudan kutoka katika hali mbaya inayopitia."
Mapigano ya silaha yalianza huko Sudan Aprili 15 mwaka jana kati ya jeshi la nchi hiyo (SAF) linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al Burhan ambaye ni kiongozi wa Sudan na wanamgambo wa Kikosi cha Usaidizi wa Haraka (RSF) ambao kamanda wao ni Hamdan Dagalo.
Mzozo huo umesababisha mzozo mkubwa zaidi wa watu waliokimbia makazi yao mwaka huu, huku Wasudan milioni 6.1 wakikimbilia maeneo mengine ndani ya nchi hiyo na watu milioni 1.5 kutafuta usalama nje ya nchi.
4235751