IQNA

Taarifa ya IRGC

Mashirika 10 hasimu ya ujasusi yamegonga mwamba katika njama dhidi ya Iran

9:25 - January 24, 2026
Habari ID: 3481839
IQNA-Shirika la Usalama la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetoa taarifa likisema, machafuko ambayo yamekuwa yakifanyika nchini Iran tangu mwishoni mwa Desemba yalikuwa sehemu ya "fitina iliyopangwa" na mashirika ya ujasusi ya nchi 10 maadui, kwa shabaha ya kuivuruga nchi kupitia vitendo vya vurugu, hujuma na kampeni za upotoshaji zilizoratibiwa kwa vyombo vya habari.

Katika taarifa yake ya tatu tangu baada ya machafuko hayo, IRGC imezungumzia "mbinu zilizotumiwa na "askari wa Imam Mahdi," ikimaanisha huduma za usalama na ujasusi, dhidi ya vibaraka wa adui" na mitandao yake nchini.

Taarifa ya Jesh la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu imesema: "Matukio hayo ya kigaidi yalipangwa katika mwendelezo wa Vita vya Siku 12 na yalifanywa haraka kutokana na taathira za kushindwa kimkakati kwa mfumo wa kibeberu."

IRGC imesema:Sehemu ya mpango mkuu wa Marekani na Uzayuni, ambayo ilibatilishwa na mashirika ya usalama ya Iran na kuwa macho watu wa Iran, ulihusisha kuundwa kwa "chumba cha amri cha adui" mara tu baada ya Vita vya Siku 12. Imesema chumba hicho cha amri, kilikuwa na mashirika kumi ya kijasusi ya uadui yaliyopewa jukumu la kutekeleza vitendo vya kigaidi nchini Iran.

Taarifa hiyo imesema: Mapitio ya nyaraka na taarifa zilizopatikana kutoka chumba hicho cha amri yameonyesha kuwa machafuko ya ndani, uvamizi wa kijeshi na harakati za makundi ya nyanjani zilikuwa mihimili mitatu ya operesheni zilizoanzishwa kutishia uwepo Iran.

Habari inayohusiana:

Shirika la Ujasusi la IRGC limesema, katika kujibu uhalifu huo lilizindua "operesheni za utambuzi na seti ya shughuli za ujasusi ili kuzuia na kudhibiti ukubwa, kina na wigo wa vitisho na machafuko."

Shirika hilo limesema operesheni hizo zilipelekea kukamatwa mamia ya watu waliohusishwa na mitandao ya kuvuruga usalama na mwongozo wa maelfu ya watu wengine walio katika mazingira magumu.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa IRGC imewatambua na kuwatumia wanachama 46 wa mtandao unaoshirikiana na mashirika ya ujasusi ya kigeni.

IRGC imeelezea machafuko ya hivi karibuni kama aina dhaifu na iliyobuniwa upya ya operesheni za pamoja za maadui wa kigeni dhidi ya mfumo wa Kiislamu na umoja wa utambulisho na jiografia ya Iran.

Imesema machafuko hayo pia yalihusisha mauaji ya raia, askari usalama, wafanyakazi wa vyombo vya sheria, na wanachama wa jeshi la kujitolea la Basij kupitia mapigano ya vurugu na umwagaji damu.

IRGC imeeleza imani kwamba, chini ya uongozi wa Amiri Jeshi Mkuu na kwa ushirikiano wa jumuiya ya taasisi za ujasusi na wananchi, Iran itashinda mipango ya maadui wa kigeni.

4329855

Kishikizo: iran ghasia
captcha