
Firas Elyaser alisema kuwa ingawa kauli za hivi karibuni zenye uhasama za Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu Ayatullah Khamenei kwa kiasi kikubwa ni za maneno tu, Waislamu, hasa wa madhehebu ya Shia hawawezi kuvumilia uchokozi wa aina hiyo.
Kwa mujibu wa Ofisi ya Habari ya Nujabaa mjini Tehran, Elyaser alikuwa akijibu matamshi ya Trump kuhusu Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Alisema kuwa licha ya tishio la Trump kuwa la maneno zaidi, Ushia hauwezi kukubali dharau au uchokozi kama huo.
“Ayatullah Khamenei ni miongoni mwa viongozi wakuu wa Waislamu wa madhehebu Shia duniani, na hata wazo la kumshambulia linaweza kubadili hali ya mambo katika eneo na duniani kote.
“Uchokozi wowote dhidi ya shakhsia huyu mtukufu utasababisha vita vikubwa. Trump anamkasirikia Kiongozi huyo kwa sababu amekwaza miradi ya Washington kwa miongo kadhaa.”
Alisisitiza kuwa machafuko ya hivi karibuni nchini Iran, kama ilivyokuwa katika vita vya siku 12 vya Juni 2025, yameshindwa.
Alisema kuwa nchini Iraq, Marekani ilitekeleza mtindo kama huo kupitia kile alichokiita “Jokers” (ghasia za Tishreen). “Mtindo huo huo ulitekelezwa Iran; lakini kosa la Marekani ni kutofahamu kuwa haina uwezo wa kufanya mapinduzi ya kijeshi au mapinduzi ya rangi nchini Iran!”
Habari inayohusiana.
Elyaser alisema kuwa Mashia wa Iraq hawataiacha Iran peke yake kwa namna yoyote ile. “Ikiwa itahitajika, tutapigana dhidi ya Marekani bega kwa bega na Wairani.”
Pia alisema kuwa harakati ya Nujaba inafuatilia kwa karibu mienendo ya Marekani nchini Iraq.
“Kuondoka kwao katika kambi ya anga ya Ain al-Asad lilikuwa ni onesho tu,” alisema, akiongeza kuwa uwepo wao katika kambi za Mkoa wa Kurdistan umeimarishwa, na kwamba Wamarekani wameanzisha kambi mpya kaskazini mwa Iraq.
4329524