iqna

IQNA

TEHRAN (IQNA)- Utafiti wa hivi karibuni umebaini kuwa Waislamu wa Marekani walitoa msaada wa dola bilioni 1.8 mwaka 2021, mwaka huo huo ambao ulishuhudia ongezeko kubwa la visa vya ubaguzi na unyanyasaji dhidi ya wafuasi wa dini hiyo ya Mwenyezi Mungu.
Habari ID: 3475178    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/04/28

TEHRAN (IQNA)- Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Marekani (CAIR) lilitoa wito wa kufunguliwa mashtaka ya uhalifu wa chuki mwanamume wa Maine anayeshukiwa kupanga kulipua misikiti huko Chicago.
Habari ID: 3474973    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/02/25

TEHRAN (IQNA)- Waislamu nchini Marekani wanataka uchunguzi ufanyike baada ya msikiti kuhujumiwa katika mji wa Waterloo jimboni Iowa.
Habari ID: 3474775    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/01/06

TEHRAN (IQNA)- Polisi katika mji wa Columbus jimboni Ohio Marekani wameanzisha uchunguzi kufuatia mauaji ya Imamu wa msikiti mmoja katika mji huo.
Habari ID: 3474730    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/12/27

TEHRAN (IQNA)- Watu wanaoaminika kuwa na chuki dhidi ya Uislamu sasa wanalenga biashara zinazomilikwa na Waislamu nchini Marekani.
Habari ID: 3474541    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/11/11

TEHRAN (IQNA)- Jumuiya na asasi za Kiislamu nchini Marekani zimesusa kuhudhuria dhifa ya kila mwaka ya Idul-Fitri inayoandaliwa na Ikulu ya White House kulalamikia uungaji mkono wa serikali ya nchi hiyo kwa jinai za kinyama za utawala haramu wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina wakiwemo wa Ukanda wa Ghaza.
Habari ID: 3473920    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/17

TEHRAN (IQNA)- Nchini Marekani kumeshuhudiwa ongezeko la asilimia 9 ya idadi ya malalamiko ya unyanyasaji dhidi ya Waislamu ambayo yalipokewa mwaka uliopita wa 2020 ikilinganishwa na mwaka wa kabla yake.
Habari ID: 3473855    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/04/27

TEHRAN (IQNA)- Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Marekani (CAIR) imepongeza hatua ya rais mpya wa nchi hiyo, Joe Biden, kuondoa marufuku ya kusafiri na kuhajiri kuelekea Marekani raia wa nchi za Kiislamu.
Habari ID: 3473580    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/01/22

TEHRAN (IQNA) -Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Marekani (CAIR), limetangaza kuwa litatenga s ofisi katika makao makuu yake kwa ajili ya kutumiwa na Taasisi ya Kupambana na Chuki Dhidi ya Uislamu au Islamophobia Ufaransa (CCIF) ambayo imefungwa na serikali ya nchi hiyo.
Habari ID: 3473423    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/05

TEHRAN (IQNA) - Mwanamke Muislamu nchini Marekani amewasilisha kesi mahakamani na kusema haki zake za kiraia na kidini zilikiukwa pale maafisa wa Idara ya Polisi ya Los Angeles (LAPD) walipomvua Hijabu (mtandio) wakati akihudhuria mkutano wa Tume ya Polisi mwaka jana.
Habari ID: 3473180    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/18

TEHRAN (IQNA) – Polisi katika jimbo la Minnesota Marekani wanawasaka vijana wawili ambao walimpiga na kumuumiza kiongozi wa Waislamu katika eneo hilo. Vijana hao wawili wanakisiwa kuwa na umri wa miaka 20 hivi na mmoja ni mzungu huku mwingine akiwa na asili ya Afrika.
Habari ID: 3473050    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/09

TEHRAN (IQNA) – Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Marekani (CAIR) limeanzisha kampeni maalumu ya kuwahimiza Waislamu kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa rais utakaofanyika nchini humo mwaka 2020.
Habari ID: 3472395    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/22

TEHRAN (IQNA) - Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Marekani (CAIR) limekosoa ujumbe wa Twitter wa Rais Donald Trump wa nchi hiyo wenye kukejeli Uislamu na Waislamu na kusema ujumbe huo unaweza kuhatarisha maisha ya Wamarekani Waislamu na Masingasinga.
Habari ID: 3472370    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/14

TEHRAN (IQNA) – Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Marekani (CAIR) limetoa ushauri kwa Wairani-Wamarekani (Wairani wenye uraia wa Marekani) baada ya kubainika kuwa wanasumbuliwa na kubaguliwa na maafisa wa usalama kufuatia matukio ya hivi karibuni katika eneo la Asia Magharibi.
Habari ID: 3472349    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/07

TEHRAN (IQNA) – Meya Mwislamu huko New Jersey nchini Marekani amesema alishikiliwa kwa muda katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa John F. Kennedy mjini New York mwezi uliopita ambapo maafisa wa usalama walimsaili kuhusu iwapo anawafahamu magaidi.
Habari ID: 3472129    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/09/14

TEHRAN (IQNA)- Waislamu katika mji wa Memphis jimboni Tenessee wameanza chehreza za muda wa mwezi moja kwa lengo la kuutmabulisha Uislamu kwa wasiokuwa Waislamu eneo hilo.
Habari ID: 3471861    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/03/04

TEHRAN (IQNA)-Waislamu Marekani wamelaani uamuzi wa Mahakama ya Kilele nchini humo kuunga mkono marufuku kuingia nchini humo wasafiri kutoka nchi tano za Waislamu huku wakisema uamuzi huo utawaathiri vibaya.
Habari ID: 3471575    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/06/28

TEHRAN (IQNA)-Baraza La Mahusiano ya Kiislamu Marekani (CAIR) limewasilisha malalamiko mahakamani baada ya kubainika kuwa wafungwa katika jimbo la Alaska wanalishwa nyama ya nguruwe katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Habari ID: 3471530    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/05/25

TEHRAN (IQNA) - Baraza la Mahusiano ya Kiislamu nchini Marekani (CAIR) limetangaza ripoti ambayo ina ushahidi unaoonyesha kuwa hatua ya utawala wa Rais Donald Trump kupiga marufuku Waislamu kutoka baadhi ya nchi kuingia nchini humo ni jambo ambalo limechangia kuongezeka chuki dhidi ya Uislamu nchini humo.
Habari ID: 3471470    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/04/18

TEHRAN (IQNA)- Serikali ya Jimbo la Texas nchini Marekani imetangaza zawadi ya $5000 kwa yeyote atakayetoa taarifa zitakazopelekea kukamatwa mtu ambaye alimdunga kisu mwanamke Mwislamu katika mji wa Houston.
Habari ID: 3471457    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/04/07