IQNA

CAIR: Anayetuhumiwa kwa njama ya kulipua Misikiti Chicago ashtakiwe

18:01 - February 25, 2022
Habari ID: 3474973
TEHRAN (IQNA)- Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Marekani (CAIR) lilitoa wito wa kufunguliwa mashtaka ya uhalifu wa chuki mwanamume wa Maine anayeshukiwa kupanga kulipua misikiti huko Chicago.

Waendesha mashtaka walimwambia jaji wa mahakama ya shirikisho Jumanne kwamba mtu huyo, ambaye alikamatwa Februari 11 kwa kumiliki vilipuzi, alipanga kutekeleza hujuma ya mabomu katika misikiti miwili huko Chicago. Mwanamume huyo pia inasemekana alipanga kulipua sinagogi. Kufikia sasa, ameshtakiwa kwa kosa moja la kupatikana na kifaa cha uharibifu ambacho hakijasajiliwa.

Katika taarifa yake, Naibu Mkurugenzi wa CAIR Edward Ahmed Mitchell alisema:

"Kesi hii ya kustuaa inaangazia tishio halisi linaloletwa na chuki dhidi ya Uislamu, chuki dhidi ya Wayahudi na aina nyinginezo za chuki. Tunashukuru mamlaka za kutekeleza sheria kwa kukomesha njama hii ya kigaidi. Tunawasihi waendesha mashtaka wa serikali na shirikisho kufuatilia mashtaka ya uhalifu wa chuki katika kesi hii, na tunahimiza vyombo vya kutekeleza sheria kote nchini kukabiliana na uhalifu unaochochewa na upendeleo.

Alisema Waislamu wa Marekani na CAIR wanasimama katika mshikamano na wale wote wanaopinga ubaguzi wa rangi dhidi ya watu wenye asili ya Afrika, chuki dhidi ya wageni, chuki ya Uislamu na chuki dhidi ya Wayahudi. Aidha amesema wanapinga itikadi potovu kuwa wazungu ndio watu bora zaidi na aina nyingine zote za ubaguzi.

3477941

Kishikizo: cair waislamu chicago
captcha