IQNA

Waislamu Amerika ya Kaskazini

Mkutano wa Kila Mwaka wa Waislamu Amerika Kaskazini wafanyika Baltimore

17:17 - May 30, 2022
Habari ID: 3475315
TEHRAN (IQNA)- Waislamu kutoka kote Marekani walimiminika katika Kituo cha Mikutano cha Baltimore kwa Mkutano wa 47 wa Mwaka wa ICNA-MAS 2022.

Mkutano huo ulianza huko Baltimorem Maryland, Jumamosi na unasimamiwa na Jumuiya ya Waislamu wa Amerika ya Kasakazini (ICNA) na Taasisi ya Waislamu wa Amerika (MAS). 

Kongamano la mwaka huu lililofanyika chini ya kaulimbiu “Kujenga Jumuiya ya Haki, Ujumbe Uendelee”, lilianza kwa usomaji mzuri wa Qur'ani Tukufu huku kikao cha kwanza cha makaribisho kikiendeshwa na Dk. Mohsin Ansari, Rami Kawas, Nihad Awad wa Baraza la Uhusiano wa Marekani na Uislamu (CAIR), Sumaira Afzal ( Wanadada wa ICNA Sisters), na wengine.

Waislamu zaidi ya 22,000 walihudhuria sherehe za ufunguzi wa Kongamano kubwa zaidi la Waislamu wa Amerika Kaskazini ambalo hufanyika kila mwaka na kuandaliwa na ICNA ambayo ni mojawapo ya jumuiya kubwa zaidi za Kiislamu katika Amerika Kaskazini.

ICNA Inaendesha miradi, programu, na shughuli nyingi ambazo zinafanyika kwa lengo la kuleta mageuzi katika jamii kwa ujumla.

Tangu 1968, ICNA imefanya kazi ya kujenga mahusiano kati ya jamii kwa kujitolea katika elimu, mawasiliano, huduma za kijamii, na juhudi za misaada.

Muslims from Across US Attend ICNA-MAS Convention 2022 in Baltimore

Muslims from Across US Attend ICNA-MAS Convention 2022 in Baltimore

3479105

Kishikizo: icna waislamu cair
captcha