IQNA

Chuki dhidi ya Waislamu

Waislamu wanyunyiziwa pilipili wakiswali katika Gereza la Missouri, Marekani

17:50 - March 04, 2023
Habari ID: 3476658
TEHRAN (IQNA) – Kesi imewasilishwa katika jimbo la Missouri nchini Marekani baada ya wanaume Waislamu waliokuwa wakisali pamoja kwenye chumba chao kwenye gereza kumwagiwa dawa ya pilipili na kushambuliwa na maafisa wa gereza

Kesi hiyo iliwasilishwa Alhamisi na Baraza la Mahusiano ya Marekani na Kiislamu (CAIR)-Missouri na dhidi ya maafisa wa Idara ya Magereza ya Missouri.

 "Kesi hii inahusu kuwawajibisha maafisa wa serikali na kuzingatia haki za raia wote," Kimberly Noe-Lehenbauer, wakili wa haki za kiraia wa CAIR, alisema katika taarifa ya habari. "Mara mtu anapoingia katika kituo cha kurekebisha tabia (gereza), hapotezi haki zake za kimsingi na huwa walengwa wazi wa ghasia na unyanyasaji."

Kwa mujibu wa shtaka lililowasilishwa, wanaume Waislamu walikuwa wameruhusiwa kusali pamoja mara nyingi katika kitengo chao cha makazi katika gereza hilo baada ya msikiti wao kufungiwa wakati wa janga la COVID-19.

Mnamo Februari 28, 2021, wanaume tisa Waislamu walipokuwa wakisali katika chumba kimoja, afisa wa gereza aliwaambia waache kusali ghafula, ingawa watu hao walikuwa wamesali pamoja mara tatu hapo awali siku hiyo, kulingana na kesi hiyo..

Wawili kati ya wanaume hao waliacha kusali na kuondoka. Wengine wawili nao waliacha kusali lakini wakafungwa pingu. Watano kati ya watu hao waliendelea kusalia na hapo walimwagiwa dawa ya pilipili.

Nyaraka zilizowasilishwa mahakamani zinaonyesha kuwa baadhi ya wanaume hao walihamishiwa katika magereza mengine bila sababu, huku wengine wakiendelea kuteswa kimwili na kudhalilishwa au kulipizwa kisasi baada ya kuwasilisha malalamiko yao.

Maafisa hao wa gereza wanaoshtakiwa wanadaiwa kukiuka haki za kikatiba za wafungwa, ikiwa ni pamoja na haki ya kuabudu, kulindwa dhidi ya adhabu ya kikatili na isiyo ya kawaida na kulindwa dhidi ya ubaguzi wa rangi.

3482695

Habari zinazohusiana
captcha