iqna

IQNA

TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amemteua Hujjatul Islam Hamid Shahriyari kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu.
Habari ID: 3472280    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/12/15

Kiongozi Muadhamu
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameshukuru harakati ya wananchi wengi wa taifa la Iran katika kipindi cha wiki moja iliyopita na kusisitiza kuwa kwa harakati hiyo wananchi wa Iran wamesambaratisha njama kubwa, hatari sana na iliyoratibiwa.
Habari ID: 3472235    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/11/27

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) – Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amelihutubu taifa la Iran pamoja na marafiki na maadui wa mapinduzi na kusisitiza kuwa, wote, wakiwemo marafiki na maadui wa mapinduzi wafahamu kuwa, kuhusiana na medani ya kijeshi, kisiasa na kiusalama -kama vitendo vya machafuko na uharibifu vilivyotokea hivi karibuni hapa nchini ambavyo havikufanywa na wananchi wa kawaida- tumemuacha nyuma adui na kwa fadhila za Mwenyezi Mungu tutamshinda adui huyu pia katika medani ya vita vya kiuchumi.
Habari ID: 3472222    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/11/20

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema mazungumzo na Marekani hayajakuwa na matokeo yoyote na kusisitiza kuwa: " "Kupiga marufuku mazungumzo na Marekani ni moja ya njia muhimu za kuwazuia kujipenyeza nchini Iran."
Habari ID: 3472199    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/11/03

Inna Lillah wa Inna Ilayhi Rajioun
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametuma salamu za rambi rambi kufuatia kuaga dunia mwanazuoni mkubwa na mwenye jitihada Hujjatul Islam wal Muslimin Sayyid Ja'far Murtada al-Amili.
Habari ID: 3472192    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/10/28

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa iwapo vijana watasimama kidete katika njia iliyonyooka na ya haki, basi wataweza kuleta mabadiliko katika taifa la Iran na dunia nzima kwa ujumla.
Habari ID: 3472180    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/10/19

Kiongozi Muadhamu katika Mkutano na Waziri Mkuu wa Pakistan
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kwa muda sasa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imewasilisha mpango wa nukta nne wa kumaliza vita nchini Yemen na kuongeza kuwa: "Iwapo vita hivyo vitamalizika ipasavyo, basi jambo hilo linaweza kuwa na taathira chanya katika eneo.
Habari ID: 3472169    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/10/13

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amepongeza msimamo imara na wa kishujaa wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusiana na uharamu wa kutumia bomu la nyuklia na kusema kuwa: Iran haiwekezi kwa ajili ya kutengeneza na kutunza bomu ya nyuklia.
Habari ID: 3472163    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/10/09

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu usiku wa kuamkia Jumatatuametuma ujumbe katika ukurasa wake wa Twitter kuhusiana na machafuko ya hivi karibuni nchini Iraq akisisitiza udharura wa kuwepo umoja na mshikamano kati ya mataifa ya Iran na Iraq.
Habari ID: 3472161    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/10/07

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria kauli mpya zilizotolewa na Marekani kuhusu mazungumzo na akasisitiza kwamba: Viongozi wote wa Jamhuri ya Kiislamu wanakubalina kwa kauli moja kuwa, hayatafanywa mazungumzo na Marekani katika ngazi yoyote ile.
Habari ID: 3472134    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/09/17

TEHRAN (IQNA) - Ismail Hania Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amemuandikia barua Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kushukuru yale aliyoyazungumza katika mkutano wake na ujumbe wa harakati hiyo uliofanya ziara hapa mjini Tehran hivi karibuni .
Habari ID: 3472110    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/09/02

TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema anasikitishwa na hali waliyonayo Waislamu wa eneo la Kashmir nchini India.
Habari ID: 3472095    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/08/22

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, Saudi Arabia na Imarati zinataka kuigawanya Yemen; na akasisitiza kwamba: Inalazimu kusimama na kukabiliana kwa nguvu zote na njama hiyo na kuunga mkono Yemen moja, iliyoungana na yenye ardhi yake yote kamili.
Habari ID: 3472083    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/08/14

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika ujumbe kwa Mahujaji
TEHRAN (IQNA) – Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ametoa wito kwa mataifa ya Waislamu kuungana kukabiliana na njama ya Marekani ya kile inachokitaja kuwa eti ni 'Muamala wa Karne' kuhusu kadhia ya Palestina.
Habari ID: 3472077    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/08/10

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) -Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: "Ustawi wa sayansi zenye faida kwa Iran ni jambo linalowezekana na ustawi huo unapaswa kuwa kwa msingi mtazamo wa kimapinduzi na fikra za Kiislamu."
Habari ID: 3472074    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/08/08

TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amebainisha msimamo wake kuhusu jinai za hivi karibuni za utawala wa kiimla wa Bahrain ambao umewanyonga kidhalimu vijana wawili wapinzani katika nchi hiyo ndogo ya Ghuba ya Uajemi.
Habari ID: 3472067    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/08/01

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amekosoa vikali misimamo ya nchi za Ulaya na kushindwa kwao kutekeleza ahadi zao ndani ya mapatano ya nyuklia ya JCPOA na kusisitiza kwa kusema: "Sisi ndio kwanza tumeanza kupunguza hadi zetu ndani ya mapatano hayo na bila ya shaka tutaendelea tu kupunguza utekelezaji wa ahadi zetu ndani ya JCPOA."
Habari ID: 3472047    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/07/18

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema serikali ya Saudi Arabia ina wajibu na majukumu mazito ya kulinda usalama wa mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu na hadhi yao bila ya kueneza anga ya kipolisi.
Habari ID: 3472031    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/07/03

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa lengo kuu la pendekezo la Marekani la kufanya mazungumzo na Iran ni kutaka kulipokonya taifa la Iran silaha na sababu za nguvu na uwezo wake.
Habari ID: 3472018    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/06/26

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: "Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haiimaini Marekani hata kidogo na uzoefu mchungu wa mazungumzo yaliyotangulia na Marekani katika fremu ya JCPOA kamwe hautarudiwa tena kwani hakuna taifa lolote huru na lenye akili litakubali kufanya mazungumzo chini ya mashinikizo."
Habari ID: 3472000    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/06/13