IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
17:21 - October 07, 2019
News ID: 3472161
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu usiku wa kuamkia Jumatatuametuma ujumbe katika ukurasa wake wa Twitter kuhusiana na machafuko ya hivi karibuni nchini Iraq akisisitiza udharura wa kuwepo umoja na mshikamano kati ya mataifa ya Iran na Iraq.

Ayatullah Ali Khamenei amesema kuwa Iran na Iraq ni mataifa mawili ambayo miili, nyoyo na roho zao zinaunganishwa pamoja na imani ya Mwenyezi Mungu na kuwapenda Ahlubaiti wa Mtume Muhammad (saw) na Hussein bin Ali (as); muungano na mfungamano huo utapanuka zaidi siku baada ya nyingine," 

Ayatullah Khamenei ameongeza kuwa: "Maadui wanafanya njama za kuzusha mifarakano lakini wameshindwa na njama na hila hizo zitagonga mwamba." 

Katika siku za hivi karibuni baadhi ya maeneo ya Iraq ukiwemo mji mkuu, Baghdad, yalishuhudia maandamano makubwa ya wananchi wakilalamikia hali mbaya ya huduma za umma, ukosefu wa ajira na ufisadi katika idara za serikali.

Maandamano hayo yamezimwa baada ya Waziri Mkuu wa Iraq, Adil Abdul-Mahdi kutangaza awamu ya kwanza ya utekelezaji wa matakwa ya wananchi. 

Ushahidi unaonyesho kuwa maandamano hayo ya hivi karibuni nchini Iraq hayakuanzishwa na wananchi bali yalichochewa na maadui kutoka nje ya nchi.

Hussein al Asadi ambaye ni miongoni mwa viongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Iraq amesema kuwa, serikali ya Marekani inahusika na machafuko ya sasa nchini humo kutokana na kutoridhishwa kwake na siasa za serikali ya Baghdad.

Vilevile imedokezwa kuwa asilimi 79 ya jumbe zote za Twitter ambazo zimesambazwa kuhusu maandamano ya Iraq zilienezwa na watumiaji wa Twitter walioko Saudi Arabia.

3469589

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: