TEHRAN (IQNA)- Ayatullah Sayyed Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametuma salamu za rambi rambi kufuatia kuaga dunia mwanazuoni mujahidi na mwanamapinduzi marhum Ayatullah Ibrahimi Amini ambaye pia alikuwa mwanachama wa Baraza la Wanazuoni Wanaomchagua Kiongozi Muadhamu.
Habari ID: 3472702 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/25
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametuma ujumbe maalumu wa kulishukuru na kulipongeza utendaji kazi wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC.
Habari ID: 3472692 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/22
TEHRAN (IQNA) – Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyed Ali Khamenei amejibu swali (Istifta) kuhusu Saumu ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani katika mazingira ya sasa ya kuenea janga la COVID-19 au corona duniani.
Habari ID: 3472682 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/19
Kiongozi Muadhamu katika hotuba ya Idi ya Nisf Shaaban
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema hitajio la kina na pana la mwanadamu wa leo la kuwa na mkombozi halina kifani katika historia.
Habari ID: 3472649 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/04/09
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, mpango wa kuwachunguza watu kiafya nchini Iran kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19 au kirusi cha corona ni kazi kubwa ya kujivunia.
Habari ID: 3472612 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/29
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amewashukuru wananchi kwa kuufuzu kwa kiwango cha kuridhisha mtihani mkubwa wa uchaguzi na kuweza kuzima propaganda za kila upande za maadui na kutumia kwao vibaya suala hilo na akasisitiza kwamba: Taifa zima linapaswa kuwa macho na kujiweka tayari kukabiliana na njama za adui zinazolenga kutoa pigo kwa mihimili tofauti ya nchi.
Habari ID: 3472499 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/23
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu mapema leo asubuhi, amepiga kura katika dakika za awali kabisa za kuanza zoezi la upigaji kura za uchaguzi wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na uchaguzi mdogo wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu Wanaomchagua Kiongozi Muadhamu.
Habari ID: 3472491 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/21
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyed Ali Khamenei amesema Marekani itazama kama ilivyozama ile meli kubwa maarufu ya Titanic.
Habari ID: 3472484 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/18
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuhusu mahudhurio makubwa ya wananchi imara wa Iran katika maandamano ya Bahman 22, na katika kuusindikiza mwili wa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, kwamba uthabiti mkubwa wa taifa la Iran wa kuyakabili mashinikizo makubwa na ya kinyama ya Marekani umewastaajabisha wafuatiliaji wa masuala ya kimataifa.
Habari ID: 3472474 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/15
TEHRAN (IQNA) - Ismail Haniya Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amemtumia ujumbe Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na akimpongeza yeye na taifa la Iran kufuatia maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Habari ID: 3472463 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/12
AMIRI JESHI MKUU WA IRAN
TEHRAN (IQNA) - Amiri Jeshi Mkuu wa vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, kuna ulazima wa Iran kuwa na nguvu katika pande zote hasa katika uga wa ulinzi; na akasisitiza kwamba: "Ni lazima kuwa na nguvu ili vita visiibuke na vitisho viishe."
Habari ID: 3472451 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/08
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, mpango wa Marekani uliopachikwa jina la Muamala wa Karne utakufa hata kabla ya Trump mwenyewe kufa na kuongeza kuwa, njia ya kukabiliana na mpango huo ni kusimama kidete na kufanya jihadi kishujaa taifa na makundi ya Palestina pamoja na uungaji mkono wa ulimwengu wa Kiislamu kwa taifa hilo.
Habari ID: 3472444 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/05
Kiongozi Muadhamu katika ujumbe kwa Kikao cha 54 cha Umoja wa Jumuia za Kiislamu za Wanachuo wa Ulaya
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametuma ujumbe kwa Kikao cha 54 cha Umoja wa Jumuia za Kiislamu za Wanachuo wa Ulaya akiwasisitizia kwamba, kikao chao mwaka huu kinafanyika baada ya kutokea matukio muhimu na kila moja ya matukio hayo linaonesha ukubwa na itibari ya Iran ya Kiislamu na taifa la kimapinduzi.
Habari ID: 3472406 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/25
Kiongozi Muadhamu
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amefafanua kuhusu misingi ya fikra za Kiislamu na malengo yake kukiwemo kusimama imara kwa Jamhuri ya Kiislamu na kusema hiyo ni nukta inayoivutia dunia.
Habari ID: 3472390 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/20
TEHRAN (IQNA) -Hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa jana mjini Tehran, imeakisiwa sana na vyombo vya habari vya kigeni.
Habari ID: 3472382 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/18
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
THERAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema pigo la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) kwa adhama ya Marekani ni jambo ambalo limepelekea nchi hiyo ifedheheke na kuongeza kuwa: "Pigo hilo kubwa na lenye nguvu haliwezi kufidiwa kwa chochote na hivyo hatua ya hivi karibuni ya Marekani ya kuongeza vikwazo haiwezi kuondoa fedheha hiyo."
Habari ID: 3472379 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/17
TEHRAN (IQNA) – Mwanazuoni wa ngazi za juu wa Mashia wa Iraq, Ayatullah Sayyed Ali al-Sistani amemtumia risala ya rambirambi Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyed Ali Khamenei kufuatia kuuawa shahidi kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu Liteni Jenerali Qassem Soleimani.
Habari ID: 3472338 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/05
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinzudi ya Kiislamu akibainisha kwamba, 'Mimi, serikali na taifa la Iran tunalaani vikali shambulizi la Marekani dhidi ya Hashdu sh-Sha'abi ya Iraq', amesisitiza kuwa, watu wa eneo hili wanaichukia sana Marekani.
Habari ID: 3472324 Tarehe ya kuchapishwa : 2020/01/01
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, suala la kuwaenzi mashahidi ni jambo la lazima na ni jukumu la kila mtu kwani hivi sasa kuna siasa na harakati za kikhabithi zinazolenga kusahaulisha nembo za Mapinduzi ya Kiislamu hususan utamaduni wa jihadi na kuwa tayari kujitolea kufa shahidi katika njia ya Allah.
Habari ID: 3472308 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/12/27
Kwa mnasaba wa Krismasi
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amewanasihi wafuasi wa dini ya Kikristo wafungamane na vitendo vyema kama walivyoelekezwa na Nabii Issa Masih (Amani ya Mwenyezi Mungu Iwe Juu Yake-AS-).
Habari ID: 3472302 Tarehe ya kuchapishwa : 2019/12/25