IQNA

Kiongozi Muadhamu
22:18 - November 27, 2019
News ID: 3472235
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameshukuru harakati ya wananchi wengi wa taifa la Iran katika kipindi cha wiki moja iliyopita na kusisitiza kuwa kwa harakati hiyo wananchi wa Iran wamesambaratisha njama kubwa, hatari sana na iliyoratibiwa.

Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo amekutana na kuzungumza na maelfu ya vikosi vya kujitolea vya wananchi (Basij) na kupongeza wiki ya Basij. Katika mjumuiko huo wa vikosi hivyo vya kujitolea vya wananchi, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria  njama ya maadui ya kutekeleza mkakati wao wa hivi karibuni na kueleza kuwa maadui hao walitumia gharama kubwa sana katika njama yao hiyo na walikuwa wakisubiri fursa ambapo walistafidi na vitendo vya uharibifu, kuua watu na kutekeleza vitendo vya shari, na walidhani kwamba suala la mafuta ya petroli ni fursa nzuri kwao; na ndipo wakaingiza genge lao katika maidani hata hivyo wananchi wa Iran wameweza kuisambaratisha harakati hiyo ya adui kwa umoja wao mkubwa. 

Ayatullah Khamenei amesisitiza kuwa harakati adhimu ya wananchi wa Iran katika miji mbalimbali ni pigo kali kwa uistikbari na Uzayuni wa kimataifa; jambo lililozipelekea pande hizo kurudi nyuma.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameutaja mfumo wa kibeberu kuwa ni adui kwa wananchi wote wa Iran  na kueleza kuwa:  Basij ni kikosi chenye umuhimu mkubwa  kwa wananchi na nchi kwa ujumla, na ndio maana kikawa kinakabiliwa vikali na njama za kila aina za maadui; hata hivyo hakuna shaka kuwa Basij itaibuka na ushindi katika uhasama na njama hizo dhidi yake.

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Ayatullah Khamenei amezungumzia suala la vitisho vinavyoikabili nchi hii na kwa nini Mfumo wa Kiislamu siku zote unakabiliwa na vitisho na kueleza kuwa: Mfumo wa Kiislamu umetokana na misingi na thamani za Kiislamu; na Uislamu pia ni mbeba bendera ya uadilifu na uhuru.

Itakumbukwa kuwa hivi karibuni, wiki mbili ziliz, serikali ya Iran iliamua kukata ruzuku ya mafuta ya petroli iliyokuwa ikiitoa. Pamoja na kuondolewa ruzuku hiyo, bado Iran ni miongoni mwa nchi ambazo bei ya mafuta ya petrol ni ya chini zaidi duniani ambapo kwa sasa lita moja ya petroli kwa watumizi wa kawaida ni takribani senti 13 za Kimarekani. Maandamano ya kulalamikia hatua hiyo yalitumiwa vibaya na wahuni ambao waliibua ghasia na machafuko na kuteketeza mali ya umma na ya watu binafsi. Serikali ya Iran imetangaza kuwa fedha zitakazopatikana baada ya kuondolewa ruzuku zitatumika kuwasaidia watu wenye kipato cha chini katika jamii. Waziri wa Mafuta Iran Bijan Namdar Zanganeh amesema hatua ya kuongezwa bei ya amfuta ya petrol imepelekea kupungua matumizi ya bidhaa hiyo kwa lita milioni 20 kwa siku. 

3859897

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: