IQNA

Inna Lillah wa Inna Ilayhi Rajioun
14:21 - October 28, 2019
News ID: 3472192
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametuma salamu za rambi rambi kufuatia kuaga dunia mwanazuoni mkubwa na mwenye jitihada Hujjatul Islam wal Muslimin Sayyid Ja'far Murtada al-Amili.

Katika ujumbe wake, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema mwanazuoni huyo  mkubwa ameandika vitabu vingi kwa msingi wa utafiti wa kina kuhusu historia ya mwanzo wa Uislamu na mbinu yake ya uandishi ilikuwa ya kiwango cha juu. Amesema Allamah Sayyid Ja'far Murtada al-Amili aliuhudumia  umma wa Kiislamu  kwa vitabu vyake na kukidhi mahitajio muhimu ya kiutamaduni.

Ayatullah Khamenei ametuma salamu za rambi rambi kwa familia ya Marhum Allamah Ja'far Murtada na pia kwa wanazuoni wote wa Lebanon na amemuomba Mwenyezi Mungu SWT amrehemu na amghufurie Sayyid Ja'far Murtada.

Allamah Al-Sayyid Jaʿfar Murtaḍa al-Amili alikuwa miongoni mwa wanazuoni wakubwa katika vyuo vya kidini nchini Lebanon na mjini Qum, Iran na alibobea katika historia ya Uislamu na madhehebu ya Shia. Allamah Al-Sayyid Jaʿfar Murtaḍa al-Amili aliaga dunia 26 Oktoba  wakati akipata matibabu hospitalini mjini Beirut. Alikuwa na umri wa miaka 74 wakati alipoaga dunia.

Kati ya vitabu vingi alivyoandika kuhusu historia ya Uislamu na itikadi za Kishia tunaweza kutaja Al-Sahih min sirat al-Nabi al-A'zam, Ma'sat al-Zahra' (a), Al-Sahih min sirat al-Imam 'Ali (a), Al-Ziwaj al-muwaqqat fi l-Islam "al-Mut'a" (dirasat wa tahlil), Al-Wilaya al-tashri'iyya, Al-Shahadat al-thalitha fi l-adhan wa l-iqama (shubahat wa rudud), Marasim 'Ashura (shubahat wa rudud) , Mizan al-haqq na Tafsir ya Sura Hal Ata.

/3852934/

Name:
Email:
* Comment: