iqna

IQNA

TEHRAN (IQNA)- Maelfu ya wananchi wa Jordan wameandamana wakilalamikia mpango wa serikali ya nchi hiyo kutiai saini mapatano mapya na utawala haramu wa Israel unaotenda jinai kila uchao dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina.
Habari ID: 3474606    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/11/27

TEHRAN (IQNA)- Chama katika muungano tawala nchini Morocco kimepata pigo kubwa katika uchaguzi wa Bunge, kulingana na matokeo ya muda yaliyotangazwa na Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo ya kaskazini mwa Afriika.
Habari ID: 3474275    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/09/09

TEHRAN (INQA)- Algeria inasema misitu nchini humo imeteketezwa moto hivi karibuni na makundi mawili ambavyo ni ya "kigaidi", na moja ya kati ya makundi hayo linaungwa mkono na Morocco na utawala wa Kizayuni Israel.
Habari ID: 3474208    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/08/20

TEHRAN (IQNA)- Katika safari yake ya kwanza nchini Morocco tangu nchi hiyo ya Kiafrika ianzishe uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa utawala huo ghasibu amefungua rasmi ofisi za ubalozi wa utawala huo mjini Rabat.
Habari ID: 3474185    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/08/13

TEHRAN (IQNA)- Msemaji wa Harakati ya Jihad al Islami ya Palestina amelaani vikali safari ya Waziri wa Mambo ya Nje wa utawala haramu wa Israel nchini Morocco na kubainisha kuwa, ziara hiyo haikubaliki.
Habari ID: 3474182    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/08/12

TEHRAN (IQNA)-Vijana ambao waliwakilisha Ghana katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani yaliyoandaliwa Morocco na Taasisi ya Mfalme Mohammad VI ya Maulamaa Waafrika wametunukiwa zawadi.
Habari ID: 3473997    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/06/11

TEHRAN (IQNA)- Maelfu ya watu wa Morocco wameanzisha kampeni katika mitandao ya kijamii kwa lengo la kulaani jinai za kinyama za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Ukanda wa Ghaza huku wakitaka nchi yao ikato uhusino na utawala huo bandia.
Habari ID: 3473982    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/06/06

TEHRAN (IQNA)- Serikali ya Morocco imetangaza kuwa itatekeleza sheria ya kutotoka nje usiku katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka huu nchini humo.
Habari ID: 3473797    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/04/09

Jumuiya ya Maulama wa Kiislamu Duniani
TEHRAN (IQNA)- Jumuiya ya Kimataifa ya Maulamaa Waislamu (IAMS) amesema kuwa, viongozi wanaotaka mapatano wameanzisha uhusiano wa kawaida na Israel kwa sababu ya woga, tamaa na kwa ajili ya kulinda maslahi yao pamoja na tawala zao, hatua ambayo ni haramu na batili.
Habari ID: 3473502    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/28

Harakati ya Kiislamu ya Amal ya Jordan
TEHRAN (IQNA) – Harakati ya Kiislamu ya Amal ya Jordan imetoa taarifa na kusema hatua ya Morocco kuafiki kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel ni kashfa kubwa na pia ni uhaini wa kihistoria.
Habari ID: 3473491    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/25

TEHRAN (IQNA) - Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kitendo cha baadhi ya nchi za Kiarabu cha kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel ni kuwasaliti wananchi wa Palestina na umma wa Kiislamu kwa ujumla.
Habari ID: 3473488    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/24

Tunisia imesema haina mpango wowote wa kuchukua uamuzi sawa na wa Morocco wa kuanzisha uhusiano na utawala bandia wa Israel.
Habari ID: 3473457    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/15

TEHRAN (IQNA)- Waziri Mkuu wa Algeria amekosoa hatua ya Morocco kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3473450    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/12

TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imelaani vikali 'mapatano' ya kuanzishwa uhusiano wa kawaida baina ya Morocco na utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3473448    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/12

TEHRAN (IQNA) - Harakati za kupigania ukombozi wa Palestina zimelaani vikali hatua ya Morocco kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3473444    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/11

Msikiti wa Kutubiyaa, ni msikiti mkubwa zaidi katika mji wa Marakesh, nchini Morocco na pia ni moja kati ya misikiti muhimu zaidi nchini humo.
Habari ID: 3473424    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/05

TEHRAN (IQNA) - Mfalme Mohammad VI wa Morocco amesema nchi yake itaendelea kuunga mkono Wapalestina hadi watakaporejeshewa haki zao zote hasa kuanzishwa nchi huru ya Palestina mji wake mkuu ukiwa ni Quds (Jerusalem) Mashariki.
Habari ID: 3473411    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/12/01

TEHRAN (IQNA) – Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu Morocco imetangaza kuruhusia tena swala ya Ijumaa kuswaliwa katika misikiti ya nchi hiyo kuanzia Ijumaa ya wiki hii.
Habari ID: 3473259    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/10/14

TEHRAN (IQNA) – Wizara ya Wakfu ya Morocco imetangaza kupiga marufuku tena swala za Ijumaa nchini humo kutokana na kuenea tena kwa kasi ugonjwa wa corona au COVID-19 nchini humo.
Habari ID: 3473191    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/09/21

TEHRAN (IQNA) - Waziri Mkuu wa Morocco Saad Eddine El Othman amesema nchi yake inapinga kuanzisha uhusiano wowote na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3473098    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/08/24