IQNA

Mapambano dhidi ya Israel

Waandishi habari wa Morocco wataka televisheni ya Israel ya i24 iondoke nchini humo

15:53 - June 14, 2022
Habari ID: 3475374
TEHRAN (IQNA)- Waandishi wa habari wa Morocco wamepinga kufunguliwa nchini humo ofisi za televisheni ya utawala haramu wa Israel ya i24 na wametaka zifungwa mara moja.

Katika taarifa, waandishi habari hao wamelaani harakati za chombo hicho cha habari cha Kizayuni nchini humo na kuanzishwa uhusiano wowote wa kawaida na vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Aidha wamesema uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni ni jinai dhidi ya Wapalestina, taifa la Morocco na ubinadamu kwa ujumla.

Makumi ya waandishi habari kutoka vyombo mbali mbali vya habari nchini Morocco wametia saini taarifa hiyo.

Aidha wamesema kufunguliwa ofisi ya Kanali ya i24 nchini kuna lengo la kuchochea hisia za Wamorocco ambao wanitazama kadhia ya ukombozi wa ardhi za Palestina zinazokoloniwa na Israel kuwa ni suala la kitaifa. Hivi karibuni i24 ilitangaza kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa imefungua ofisi mbili nchini Morocco.

Mwezi Disemba mwaka 2020 Morocco ilijiunga na UAE, Bahrain na Sudan katika kuanzisha uhusiano rasmi na utawala haramu wa Israel chini ya upatanishi wa Marekani. Mapatano hayo yanaendelea kulaaniwa ndani ya nchi hizo za Kiarabu na ulimwengu wa Kiislamu kwa ujumla kwani ni usaliti kwa malengo matukufu ya ukombozi wa Palestina.

 

4064091

captcha