IQNA

Tunisia haina mpango wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel

17:35 - December 15, 2020
Habari ID: 3473457
Tunisia imesema haina mpango wowote wa kuchukua uamuzi sawa na wa Morocco wa kuanzisha uhusiano na utawala bandia wa Israel.

Katika taarifa, Waziri Mkuu wa Tunisia Hichem Mechichi amesisitiza kuwa nchi yake haina ajenda ya  kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Wiki iliyopita, Morocco ilikuwa nchi ya nne ya Kiarabu kuanzisha uhusiano na Israel tokea mwezi Agosti wakati mtawala wa Marekani anayeondoka, Donald Trump alipoanzisha mkakati wa kuzishinikiza nchi za Kiarabu kuanzusha uhusiano na utawala huo bandia.

Mbali na Morocco, nchi zingine za Kiarabu ambazo zimeanzisha uhusiano na Israel hivi karibuni ni pamoja na Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain na Sudan ambazo zimeanzisha uhusiano na utawala huo dhalimu katika fremu ya njama za Marekani-Kizayuni za kudhoofisha uungajo mkonowa nchi za Kiarabu kwa harakati za kupigania ukombozi wa Palestina. Nchi za Kiarabu ambazo zimekuwa na uhusiano na Israel kwa muda mrefu ni Jordan na Misri.

Mechichi aidha amesema Tunisia haijatakiwa na Marekani kuanzisha uhusiano na Israel.

Algeria imechukua msimamo mkali  na kulaani vikali hatua ya Morocco kuanzisha uhusiano na utawala wa Israel mkabala wa Washington kutambua mamlaka ya Morocco katika eneo la Sahara Magharibi ambalo limejitangazia uhuru kutoka Rabat.

Marekani imesema itatambua mamlaka ya Morocco katika eneo la Sahara Magharibi la nchi hiyo ambalo limejitangazia uhuru. Ufalme wa Morocco umetangaza kuwa Marekani hivi karibuni itafungua ubalozi mdogo huko Sahara Magharibi.

Algeria ambayo unaunga mkono harakati ya Polisario inaypigania uhuru wa Sahara Magharibi imesema hatua hiyo ya Morocco ni katika fremu ya njama za kigeni za kuvuruga uthabiti wake.

Harakati kaadhaa za kupigania ukombozi wa Palestina zimetoa taarifa na kulaani hatua ya Morocco kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel na kusema huo ni usaliti wa wazi kwa Wapalestina. Aidha harakati hizo zimesema kufuatia usaliti huo, Morocco haistahiki tena kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Quds (Jerusalem) ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu.

3473418

 

captcha