Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Kimataifa la Habari za Qur'ani IQNA, kauli hiyo ya Baraza la Mahusiano ya Kiislamu la Marekani inafuatia hatua Banki ya Minnesota ya kufunga akaunti zote za fedha za Waislamu katika benki hiyo. Sali Abdallah, Mkurugenzi wa Kitengo cha Haki za Raia Katika Baraza la Mahusiano ya Kiislamu nchini Marekani amesema kuwa, baadhi ya Waislamu waliofungiwa akaunti zao za fedha katika tawi la banki hiyo wamesilimu hivi karibuni. Sali Abdallah amesisitiza kuwa, wateja Waislamu ambao wamefungiwa akaunti zao za fedha katika banki hiyo hawana historia ya kufanya uhalifu wa aina yoyote. Tayari Waislamu wa eneo hilo wamewasilisha mashtaka mahakamani dhidi ya banki hiyo wakiituhumu kukiuka haki za kiraia za Waislamu. Ikumbukwe kuwa, maisha ya Waislamu yamekuwa hatarini zaidi nchini Marekani tokea lilipotokea shambulio la Septemba 11, na Waislamu wa nchi hiyo wamekuwa wakikabiliwa na vitendo vya kibaguzi, ukandamizaji, utesaji na wengine kupigwa bila ya hatia yoyote, huku baadhi ya vyombo vya kupasha habari na hata taasisi na asasi za kiserikali za nchi hiyo zikishajiisha vitendo hivyo vilivyo dhidi ya ubinadamu.