IQNA

Kiongozi Muadhamu:Uislamu unasisitiza kuwaheshimu wafanyakazi

21:38 - April 30, 2014
Habari ID: 1401876
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwaenzi na kuwaheshimu wafanyakazi na wale wote wanaohusika katika uga wa uzalishaji ni dharura ambayo imesisitizwa na Uislamu.

Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei ametoa kauli hiyo leo matano asubuhi alipohutubia hadhara kubwa ya wafanyakazi, wakurugenzi na wataalamu wa Shirika la Mapna katika mji wa Karaj magharibi mwa Tehran ambapo ameongeza kuwa Uislamu ulitangulia kuweka misingi ya kuheshimu haki na hadhi ya mfanyakazi na wale wote walio katika sekta ya uzalishaji.

Ayatullahil Udhma Khamenei amesema mtazamo wa kuwepo mvutano baina ya mfanyakazi na mwajiri ni nukta ya pamoja ya fikra za Umaxi na Umagharibi. Amesema mtazamo huu ni ghalati na kuogeza kuwa: “Katika nyanja zote, ikiwa ni pamoja na masuala ya mfanyakazi na uzalishaji, Uislamu unasisitiza kuheshimiana, maelewano na ushirikiano. Ameongeza kuwa msingi huu unapaswa kuwa kigezo katika nyanja mbalimbali za kijamii na kiuchumi.

Kiongozi Muadhamu ameashiria vitendo vya kudhalilishwa taifa la Iran kabla ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuongeza kuwa: “Katika zama ambazo Wamagharibi walikuwa katika ujahili halisi, Iran ilikuwa imestaarabika na kuitunuku jamii ya mwanaadamu shakhsia adhimi katika nyuga za elimi na utamaduni.” Amesema Wamagharibi waporaji walieneza satwa yao mchini Iran kupitia udhalilishaji wa mabepari wa kitaghuti na hivyo kudhibiti masuala ya kiuchumi, kisiasa na kijamii nchini. Amesmea  ukweli huu mchungu ni nukta ya udhalilishaji mkubwa kwa historia ya Iran ambayo ina ustaarabu wa kale na turathi ya kubwa ya utamaduni. Ayatullahil Udhma Khamenei ameashiria kumalizika zama za kudhalilishwa taifa la Iran baada ya Mapinduzi ya Kiislamu na kusema: “Iwapo taifa la Iran linataka kupata hadhi na nafasi yake ya juu linalostahiki katika setka za kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiutamaduni na kuwa marejeo ya ustawi wa kisayansi  linapaswa kutegemea elimu, uerevu, nguvu za harakati, ubunifu na kuwa na azma imara. Kiongozi Muadhamu ameashiria msingi muhimu wa Uchumi wa Kimapambano yaani zama za ‘kutozingatia nje ya nchi na kutegemea ndani ya nchi’ na kusema: “Tunapaswa kustawi ndani ya nchi, na katika kutazama nje ya nchi tunapaswa kuwa na ushawishi katika masoko ya dunia.”

1401573

captcha