Waziri wa Waqfu wa Misri Muhammad Mukhtar Guma ambaye aliwakilisha nchi hiyo na balozi wa Morocco mjini Cairo Sayyid Muhammad Saad al Alami walitia saini makubaliano hayo kwa shabaha ya kuimarisha ushirikiano katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na kulinda nakala za hati za mkono na kubadilishana picha za nakala hizo.
Makubaliano hayo pia yanasisitiza juu ya kubadilishana uzoefu katika masuala ya kutarjumu vitabu vya Kiislamu kwa lugha mbalimbali na kufanya jitihada za kusambaza vitabu hivyo kwa lengo la kueneza mafundisho sahihi ya Uislamu.
Kipengee kingine cha makubaliano hayo kinasisitiza juu ya udharura wa kubadilishana uzefu katika masuala ya uchapishaji wa nakala za Qur’ani Tukufu na kutoa mafunzo kwa maimamu wa misikiti na kukarabati maeneo hayo.