Uamuzi huo umekuja baada ya timu ya taifa ya mpira wa kikapu ya wanawake kutoka Qatar, kuzuiwa kushiriki kwenye michuano ya mataifa ya Asia inayoendelea nchini Korea Kusini kutokana na vazi la hijabu ya Kiislamu. Taarifa iliyotolewa na FIBA imedai kuwa, sheria hiyo haikuwekwa kwa lengo la kukabiliana na dini fulani na kusisitiza kwamba, utaanza mchakato wa kuangalia uwezekano wa kuruhusiwa vazi la hijabu baada ya shirikisho hilo kupokea malalamiko kutoka nchi kadhaa.
Hatua ya FIBA ya kuizuia timu ya mchezo wa mpira wa kikapu ya Qatar kumenyana na Mongolia kwenye michuano ya Asia nchini Korea Kusini, imekosolewa vikali na baadhi ya nchi na taasisi za Kiislamu. Wachezaji wa kike wa timu ya Qatar wameeleza kuwa, kitendo hicho kimefanyika kwa lengo la kuwanyanyasa wanamichezo Waislamu.
Sheria ya marufuku ya vazi la hijabu katika mashindano ya mpira wa kikapu ilifutwa kwenye mashindano ya kitaifa, lakini bado inatumika kwenye mashindano ya kimataifa…/mh 1454333