Taarifa iliyochapishwa katika tovuti rasmi ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imelaani vikali hatua hiyo na imezitaka taasisi zote za serikali kuzuia hatua kama hizo zinazokwamisha uhusiano baina ya tamaduni mbalimbali.
Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imesema kuwa hatua hiyo inafuatia kitendo cha huko nyuma cha kudhalilisha cha kuchora vibonzo vilivyodaiwa kuwa ni vya Mtume Muhammad SAW ambavyo vilivuruga uhusiano wa Magharibi na ulimwengu wa Kiislamu. 314357