Mwandishi wa kujitolea wa IQNA ameripoti kuwa mchezo huo unaopatikana bure katika mtandao wa intaneti ambao mchezaji anapaswa kuua idadi kubwa zaidi ya Waislamu kadiri inavyowezekana, umewakasirisha Waislamu wa Australia. Waislamu hao wameituhumu serikali na polisi ya Australia kwamba wameshiriki katika kubuni mchezo huo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Urafiki ya Waislamu wa Australia Qaisar Trade amewasilisha kesi hiyo kwa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa serikali. Amesema katika barua ya mashtaka kwamba, tangu mchezo huo uzinduliwe nchini Australia, vitendo vya matusi, kuwavunjia heshima Waislamu, ubaguzi na utumiaji mabavu dhidi ya Waislamu vimekithiri.
Taasisi ya Ramadhan na Jumuiya ya Vijana wa Kiislamu wa Uingereza pia zimetoa wito wa kupigwa marufuku mchezo huo unaokebehi na kuwavunjia heshima Waislamu. 315658