IQNA

Ayatullah Khamenei: Hija, fursa adhimu ya kuwaunganisha Waislamu

14:05 - November 06, 2008
Habari ID: 1705163
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa ibada ya hija ni fursa ya umma wa Kiislamu kudhihirisha zaidi umoja na mshikamano wao.
Ayatullah Ali Khamenei amesema hayo katika mazungumzo yake na viongozi wa msafara wa hija wa wa Iran na akasema hijani fursa adhimu kwa mahujaji, umma wa Kiislamu na mfumo wa Kiislamu wa Iran na wakati bora wa kuvunja mifarakano ya kimaumbile na yanayozushwa na wanadamukati ya Waislamu na kuzikutanisha pamoja nyoyo katika ulimwengu wa Kiislamu. Ayatullah Khamenei amesema, umma wa Kiislamu siku zote unakabiliwa na mifarakano ya kimaumbile sambamba na mifarkano inayozushwa na wanadamu kutokana na kuwa na kaumu, mataifa na tamaduni tofauti na kwa msingi huo hija ni fursa adhimu kwa Waislamu kufuta mifarakano hiyo. Amesema kuwa mfumo wa Kiislamu wa Iran ni mfumo imara lakini uliodhulumiwa na akaongeza kuwa dhulma hiyo inatokana na orongo wa kimakundi, kifikra na kisisa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kwamba ukweli wa mambo kuhusu kadhia hizo unapaswa kubainishwa kwa Waislamu katika siku za ibada ya hija.
Ameashiria maisha ya amani na kidugu ya Waislamu wa madhehebu za Shia na Suni nchini Iran na utawala ulijengeka juu ya sheria za Qurani na Uislamu na akasema Waislamu katika nchi nyingi duniani wanaipenda Jamhuri ya Kiislamu, Imamu Khomeini na taifa la Iran.
Ayatullah Ali Khamenei ameashiria chuki na hasira za Waislamu kote duniani dhidi ya maadui wa dini yao na uingiliaji kati wa madola ya kibeberu hususan Marekani katika masuala yao na akasema: Waislamu wengi wanazuiwa kueleza wazi hisia zao hizo kutokana na sababu mbalimbali na kwamba Iran imekuwa jukwaa huru na la kimataifa la kutangaza malalamiko na hisia hizo za Waislamu na ndio maana inapigwa vita na Marekani. 316383
captcha