Kwa mujibu wa gazeti la Kiiraqi la al-Swabah Wairaqi 16,277 wa makundi ya Kisuni kutoka maeneo mbali mbali ya nchi hiyo walisohiriki katika uchunguzi huo wa maoni, wametoa mwito kwa vyama vya kisiasa vya Kiiraqi kutotumia nembo za kidini kwa maslahi ya kibinafsi katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa.
Uchunguzi huo wa maoni pia unaonyesha kuwa asilimia 56 ya wakaazi wa mji mtakatifu wa Najaf wamesema kuwa watawapigia kura watu watakaokuwa katika mirengo ya kidini.
Wakati huo huo, ofisi ya Ayatullah Sayyed Ali Sistani Kiongozi (Marajaa) wa Mashia wa Iraq imetangaza kuwa haiungi mkono chama chochote au kundi lolote la kidini katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa nchini humo. 317146