Akizungumza hapo jana Jumapili, Afif Nablosi amesema kuwa Barack Obama, Raisi mteule wa Marekani anataka kuwasilisha sura tofauti ya Marekani kinyume na ile iliyowasilishwa na serikali inayoondoka madarakani ya Rais George Bush kupitia nara ya 'mabadiliko' lakini akaongeza kwamba nara hiyo pekee haitoshi kwa lengo la kudhamini usalama, uadilifu na amani duniani. Nablosi amehoji kuwa ni vipi rais huyo mteule anataka kusimamisha vita vya Marekani ambavyo vimesababisha umwagikaji mkubwa wa damu na mauaji na wakati huohuo kusimamisha dhulma ambayo imefanywa dhidi ya mataifa ya Kiarabu na Kiislamu, katika hali ambayo viongozi wote wa Marekani wanaamini kwamba nguvu za kijeshi tu ndizo zinaiwezesha dunia kufikia ufanisi na maendeleo? Amesema fikra hiyo potofu ndiyo imeipelekea nchi hiyo kutoweza hata kutatua matatizo ya kiuchumi yanayoikabili hivi sasa. Amesema kama kweli rais mpya wa Marekani anataka mabadiliko anapasa kufanya juhudi za kukomesha nchi yake kuunga mkono makundi na nchi za kigaidi ukiwemo utawala haramu wa Israel unaoendelea kuwakandamiza Wapalestina wasio na hatia. 317434