Kwa mujibu wa mtandao wa Intaneti wa Ma’aa, kitabu hicho kimeandikwa na John Rownman na David Dalbin na kuchapishwa na shirika la Random House la Marekani.
Sheikh Akram Sabri amesema kuwa, ‘katika kitabu hicho, waandishi wamechunguza jinai za Wanazi wa Ujerumani na katika ulinganisho potofu, wameutusi Uislamu. Wamedai kuwa eti ukatili wa Wanazi ulitokana na misingi ya mafunzo ya dini ya Kiislamu.
Khatibu wa Msikiti wa Al Aqsa ameendelea kwa kutoa mwito kwa nchi za Kiislamu na Kiarabu kuchukua hatua za haraka kuzia uuzwaji na usambazwaji wa kitabu hicho. Aidha ametaka nuskha zote za kitabu hicho zikusanywe. Sheikh Akram Sabri ameongeza kuwa, Uislamu ni dini ya usamehevu, upendo, urafiki na mwenendo wa wastani. Amesisitiza kuwa Waislamu wana jukumu la kulinda na kutetea misingi na mafunzo yenye thamani ya dini tukufu ya Kiislamu.
Mwanachuoni huyo ameelezea masikitiko yake kuwa mwaka huu wa 2008 , wachora vibonzo, wabunge na waandishi wa riwaya wenye misimamo mikali ya kufurutu mipaka katika baadhi ya nchi za Ulaya wameutusi Uislamu na Waislamu na kumvunjia heshima Mtume Mtukufu (SAW) kwa kisingizio cha uhuru wa maoni.
Mkuu wa Baraza Kuu la Kiislamu la Palestina na Khatibu wa Msikiti wa Al Aqsa aidha ameutaka Umoja wa Mataifa kutunga sheria ambayo itaharamisha matusi dhidi ya matukufu ya kidini. 317512