Mkutano huo wa kimataifa umetayarishwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za kiislamu (ISESCO), kwa kushirikiana na Jumuiya ya Kimataifa ya Ulinganiaji wa kiislamu na Umoja wa Vyuo Vikuu vya Ulimwengu wa Kiislamu.
Mkutano huo utahudhuriwa na wahadhiri wa vyuo vikuu, Wakurugenzi wa vituo vya kiutamaduni vya Kiarabu na kiislamu katika jamii za Magharibi na waandishi wa habari.
Lengo la mkutano huo limetajwa kuwa ni kuchunguza njia za kusahihisha sura isiyokuwa sahihi ya Uislamu katika vyombo vya habari vya Magharibi, kubainisha mipaka ya uhuru wa kusema na kuzivunjia heshima dini na itikadi, kufafanua thamani za kibinadamu, kiutamaduni na kihistoria zinazopatikana katika utamaduni wa Uislamu na Magharibi, kutambua rasmi haki ya kuhitilafiana katika itikadi na kusisitiza juu ya juhudi za kusimamisha uadilifu na amani kote duniani.
Malengo mengine ya mkutano huo wa kimataifa ni kuchunguza uwezo wa Waislamu wa kutoa sura sahihi ya Uislamu na Waislamu huko Magharibi, kukabiliana na makundi yanayoupiga vita Uislamu katika nchi za Ulaya na kuzuia wimbi la propaganda chafu dhidi ya duni hiyo tukufu katika vyombo vya mawasiliano ya umma vya Magharibi. 320993