IQNA

Uchunguzi kuhusu "Kuwapa Himaya watoto kwa mtazamo wa Kiislamu"

12:54 - November 20, 2008
Habari ID: 1710457
Kongamano la kuchunguza "Kuwapa Himaya watoto kwa mtazamo wa Kiislamu" limefanyika katika ukimbi wa kitivo cha tiba katika chuo kikuu cha mkoa wa Balkh nchini Afghanistan.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA nchini Afghanistan, kongamano hilo limehudhuriwa na wahadhiri wengi wa vyuo vikuu, wasomi, wanazuoni wa kidini na wanachuo kutoka mji wa Mazar-e-Shariff.
Kongamano hilo limechunguza kadhia ya kuteswa watoto katika jamii ya leo Afghanistan na njia za kuzuia jambo hilo. Aidha washiriki wamejadili umuhimu wa kuzingatiwa mafunzo ya dini ya Kiislamu.
Kongamano hilo limefanyika kupitia uungaji mkono wa Taaisi ya Kuwalinda Watoto SABA kwa ushirikiano wa taasisi kadha za ndani ya nchi na kimatiafa.
Mwaka huu wa 2008 kumeshuhudiwa kesi nyingi kuhusu unyanyasaji na utesaji watoto katika mahakama za Afghanistan. Wataalamu wanasema, suala hili linatokana na wazazi kutofahamu ipasavyo haki za mtoto katika Uislamu. Aidha wanaowasafirisha wanaadamu kwa njia haramu wamelaumiwa kwa hali hiyo iliyojitokeza Afghanistan. 322690

captcha