IQNA

Jumuiya za Kiislamu za Indonesia zataka kutiwa nguvuni waliomvunjia heshima Mtume Muhammad SAW

12:32 - November 22, 2008
Habari ID: 1711059
Jumuiya za Kiislamu za Indonesia zimetoa wito wa kutiwa nguvuni na kuchukuliwa hatua kali watu waliohusika na maonyesho ya picha zinazomvunjia heshima Mtume Muhammad SAW katika weblogu moja ya Kiindonesia.
Mwandishi wa IQNA ameripoti kuwa Msemaji wa Polisi ya Indonesia ameahidi kuchukua hatua kali baada ya malalamiko yaliyotolewa na jumuiya za Kiislamu za nchi hiyo.
Wakati huo huo Waziri wa Habari na Mawasiliano wa Indonesia amesema wizara yake inafanya jitihada za kufuatilia maudhui hiyo na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wahalifu hao.
Wizara ya Habari ya Mawasiliano ya Indonesia Jumanne iliyopita iliyataja maonyesho ya picha hizo zinazomvunjia hesmima Mtume Muhammad SAW kuwa hayafai na kuzitaka weblogu zote nchini humo kufuta picha hizo.
Msemaji wa wizara hiyo amesema, maonyesho ya picha hizo yamewavunjia heshima Waislamu na wafuasi wa dini zote za Mwenyezi Mungu. 323506
captcha