Ummu Aiman al Faki Bashir mtafiti wa masuala ya Qur’ani wa Sudan ambaye alishiriki kwenye Kongamano la Kimataifa la Qur’ani Tukufu la Wanawake wa Kiislamu nchini Iran amemwambia mwandishi wa IQNA kwamba serikali ya Iran inajali mno suala la kuaisisi vyuo vikuu na skuli za mafunzo ya Qur’ani ambazo zinashughulikia sayansi ya kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu.
Bibi Ummu Aiman ameashiria Chuo Kikuu cha Jamiatul Mustafa ambacho amesema, ni miongoni mwa neema kubwa ambazo Mwenyezi Mungu ameitunuku Iran.
Akijibu swali kuhusu sababu ya kuwepo mahafidhi wengi wa Qura’ani ambao wanakadiriwa kuwa zaidi ya milioni tatu huko Sudan, Bibi Ummu Aiman amesema: Kuhifadhi Qur’ani nchini Sudan hakuhusishwi na umri wala tabaka makhsusi la watu na watu wote wanawake kwa wanaume na watoto wadogo wanajihusisha na kazi hiyo. Amesema kuwa huko Sudan kuna chuo kikuu kinachojulikana kwa jina la Chuo Kikuu cha Qura’ni vituo na jumuiya mbalimbali za Qur’ani na vituo vinavyojulikana kwa jina la ‘Khalwa’ makhsusi kwa kazi ya kuhifadhisha Qur’ani Tukufu.
Mhadhiri huyo wa vyuo vikuu nchini Sudan amesema kuwa kwa sasa ulimwengu wa Kiislamu unahitajia umoja na mshikamano kuliko wakati wowote mwingine. 325101