IQNA

Iraq yajitayarisha kwa Misafara ya Mazishi ya Kiongozi Shahidi mijini Najaf na Karbala

18:02 - June 29, 2026
Habari ID: 3482419
IQNA – Kufuatia kuanza kwa uratibu mpana kati ya taasisi za Iraq na Iran, Iraq inajitayarisha kuandaa misafara ya mazishi ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Shahidi Ayatullah Seyed Ali Khamenei katika miji mitakatifu ya Najaf na Karbala.

Inatarajiwa kuwa zaidi ya watu milioni moja watahudhuria hafla za mazishi katika miji hiyo miwili mitakatifu.

Kwa mujibu wa Al‑Ahed News, kwa sasa Iraq inashuhudia maandalizi makubwa kwa ajili ya kufanyika kwa mazishi ya kihistoria ya kiongozi huyo.

Shughuli za mazishi zimepangwa kufanyika tarehe 8 Julai, kwa uratibu kati ya taasisi mbalimbali za Iraq na pande za Iran, ikiwemo Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Baghdad.

Vyanzo vilivyo karibu na ubalozi wa Iran mjini Baghdad vimetangaza kuwa mwili mtukufu wa kiongozi huyo utaingia Iraq tarehe 8 Julai kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Najaf. Hafla rasmi ya mapokezi itafanyika katika uwanja huo kwa kuhudhuriwa na maafisa wa Iraq pamoja na shakhsia wa kidini, kijamii na kisiasa.

Baada ya hapo, mwili huo utapelekwa katika haram takatifu ya Imamu Ali (AS) kwa ajili ya hafla ya kuaga. Kisha msafara wa mazishi utaelekea Karbala, ambako hafla ya Khitma ya umma itafanyika katika eneo la Bain‑ul‑Haramain kwa ushiriki wa idadi kubwa ya wananchi. Hatimaye mwili huo utarudishwa tena katika Uwanja wa Ndege wa Najaf na kutoka hapo kusafirishwa kwenda mji mtakatifu wa Mashhad.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, usimamizi wa haram tukufu ya Imamu Ali (AS) mjini Najaf, pamoja na haram za Imamu Hussein (AS) na Hadhrat Abbas (AS) mjini Karbala, magavana wa Najaf na Karbala, wizara za usafiri, mambo ya ndani na mambo ya nje za Iraq, vikosi vya Hashd al‑Shaabi (PMU), pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu wa Iraq ni miongoni mwa taasisi zinazoratibu na kusimamia hafla hizo.

Takribani raia milioni moja wa Iraq kutoka mikoa mbalimbali ya nchi hiyo wanatarajiwa kushiriki katika hafla hizo za Khitma na kuuaga mwili wa Shahidi Imam Khamenei. Viongozi mashuhuri wa kidini, kisiasa, kikabila, kitamaduni na kitaaluma wa nchi hiyo pia watahudhuria tukio hilo la kihistoria.

Mbali na hafla za Najaf na Karbala, mamia ya maelfu ya mahujaji wa Iraq pia wanatarajiwa kuelekea Iran kushiriki katika hafla za mazishi zitakayofanyika kati ya tarehe 4 hadi 9 Julai katika miji ya Tehran, Qom na Mashhad.

Katika muktadha huo, taasisi husika nchini Iran na Iraq tayari zimeanza uratibu muhimu ili kurahisisha safari za mahujaji kupitia mipaka ya nchi kavu na viwanja vya ndege.

3498011

Habari zinazohusiana
captcha