IQNA

Uhusiano wa Lebanon na Iran una misingi ya kiroho, kitamaduni na kidini.

12:10 - November 26, 2008
Habari ID: 1712946
Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Kuu la Waislamu wa Kishia la Lebanon amesema kuwa urafiki wa nchi hiyo na Iran ni wa miaka mingi na unasimama juu ya misngi ya kiroho, kidini na kitamaduni.
Sheikh Abdul Amir Qublan ambaye alikuwa akizungumzia safari ya Rais Michael Sulaiman wa Lebanon nchini Iran, amesema Iran ni nchi rafiki na jirani na ina uhusiano sawa wa kidini na Waislamu na Wakristo wa Lebanon.
Sheikh Qublan amesema kuwa safari ya Rais wa Lebanon nchini Iran ina maslahi kwa mataifa yote mawili. Naibu Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Mashia wa Lebanon amemshauri Rais wa nchi hiyo kufanya kila awezalo katika safari hiyo kutetea maslahi ya Lebanon.
Rais Michael Sulaiman aliwasili nchini Iran Jumatatu ya wiki hii akiongoza ujumbe wa ngazi za juu wa nchi yake kwa lengo la kustawisha uhusiano wa pande mbili na kuchunguza hali ya mambo katika nchi za Lebanon, Palestina na eneo zima la Mashariki ya Kati kwa ujumla. 325583
captcha