Abdullah Badawi ameyasema hayo katika sherehe za kufungua Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Nilai na kuongeza kuwa njia pekee ya maendeleo ya vijana wa Malaysia ni kufanya juhudi za kielimu. Amesema, anaamini kwamba hakuna kizuizi chochote mbele ya vijana wa Malaysia kukariri mafanikio ya ustawi wa Uislamu.
Waziri Mkuu wa Malaysia ametoa wito wa kutayarishwa mazingira bora zaidi na ya kisasa kwa ajili ya kueneza elimu kati ya vijana na akazihimiza taasisi za kielimu za nchi hiyo kutoa kipaumbele zaidi kwa masomo yanayokidhi mahitaji ya jamii.
Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Nilai kilifunguliwa Jumanne ya wiki hii kwa shabaha ya kukuza kiwango cha taaluma za Kiislamu na kusisitiza juu yamatumizi ya teknolojia ya kisasa katika masomo na utafiti wa Kiislamu.
Chuo hicho kina vitengo 8 ikiwa ni pamoja na kitengo cha Qur'ani na suna, sheria, uchumi, sayansi na teknolojia, tiba na lugha za kigeni. 326245