Maandamano hayo yamefanyika katika eneo la Bawwaba Fatima karibu na mpaka wa Palestina.
Kwa mujibu wa Kanali ya Televisheni ya Al Manar, maandamano hayo yamefanyika kaskazini mwa kijiji cha Kafr Kala katika eneo Marji'yun kusini mwa Lebanon. Washiriki katika maandamano hayo wamelaani vikali kimya cha nchi za Kiarabu na taasisi za kimataifa mbele ya hujuma na ukatili wa utawala ghasibu wa Israel huko Gaza.
Bi. Fatima Shahadat mkuu wa kundi la wanawake wa Hizbullah wa kundi wa wanawake wa Hizbullah kusini mwa Lebanon amehutubu katika maandamano hayo na kusema wakaza wa Lebanon wameonyesha ukakamavu, ezi na uendelevu katika mapambano dhidi ya Wazayuni. Ametoa wito kwa wakazi wa Gaza kutowategemea wanaadamu bali watawakali kwa Mwenyezi Mungu. Amesema, ushahidi umeonyesha kuwa mapambano ndio njia pekee ya kupata haki iliyopokonywa na kwamba njia pekee ya kupata ushindi ni ezi na heshima. Bi. Fatima Shahadat amesema kuwa wakazi wa Ghaza sawa na wanaharakati wa Hizbullah, watafanya maajabu kwa kuwaangamiza Wazayuni. 328392