IQNA

Stempu za Kiongozi Muadhamu akiwa katika medani za vita kutolewa zawadi kwa viongozi wa Hamas

11:04 - December 06, 2008
Habari ID: 1716241
Stempu zinazomuonyesha Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran Ayatullah Ali Khamenei akiwa katika medani za vita vya haki dhidi ya batili zitatolewa zawadi kwa viongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) Khalid Mash’al na Ismail Hania pamoja na familia za mashahidi wa Palestina.
Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni wa Kujitetea Kutakatifu cha Khorramshahr huko kusini mwa Iran Nader Daryaban amesema kuwa pamoja na stempu hizo ambazo ni nembo ya kusimama kidete kwa taifa la Kiislamu la Iran dhidi ya ukafiri wa kimataifa na dikteita Saddam Hussein, picha kubwa ya kuvutia ya Ayatullah Khamenei akiwa katika safu ya kwanza ya mapambano wakati wa mashambulizi ya Iraq dhidi ya Iran, itatolewa zawadi kwa viongozi hao.
Daryaban amesema, miongoni mwa familia za mashahidi wa Palestina zitakazopewa zawadi hizo ni pamoja na familia ya shahid Rantisi, Yahya Ayyash, Ibrahim Abu Duhaim na Sheikh Ahmad Yasin kiongozi na muasisi wa Hamas aliyeuawa shahidi na utawala ghasibu wa Israel.
Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni wa Kujitetea Kutakatifu cha Khorramshahr amepongeza kusimama imara kwa wananchi wa Ukanda wa Gaza na mashujaa wa Palestina mbele ya jinai na ukatili wa Wazayuni na akasema: kusimama imara huko ni mapambano matakatifu mapya ya kutetea dini tukufu ya Kiislamu.
Daryaban ameongeza kuwa zawadi hizo pia zitatolewa kwa Kiongozi wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrullah. 329647
captcha